Market Structure (Muundo wa soko)

LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
459
650
MARKET STRUCTURE
Kwa kiswahili huu ni muundo wa soko au aina ya soko.

Kama mfanyabiashara au mtu ambae unataka kuingia katika biashara basi ni vyema ujue aina tofauti za masoko yaliyopo na vigezo vya kuweza kuwa katika aina flani ya soko. Pia kama mnunuaji itakusaidia kujua bidhaa flani ni matokeo ya soko la aina gani.

Vitu vinavyotumika kutofautisha masoko ni kama vifuatavyo:

1. Wauzaji wa hio bidhaa kama wapo wengi au wachache au wastani?
(Number of sellers)

2. Wanunuzi kama wapo wengi au wachache au wastani?
(Number of buyers)

3. Utofauti wa bidhaa yako na ambazo zipo teari sokoni
(Product differential)

4. Mtaji wako uliotumika au unaohitajika ni mkubwa, mdogo au wastani?
(Amount of capital)

5. Vizuizi vya kuingia kwenye io biashara ni vingi au vichache?
(Barriers to entry)

6. Hio biashara ni wauzaji au wanunuzi ndio wanapanga bei?
(Price control)

Mfano:
Biashara ya kuuza chips mtaani:

1. Wauza chips ni wengi
2. Wanunuzi wa chips ni wengi
3. Hamna tofauti ya ladha
4. Mtaji ni mdogo
5. Ni rahisi kufungua kibanda cha chips
6. Bei inapangwa na wanunuaji wa chips

Karibuni kutoa mifano mingine au maoni.

#marketstructure #barriertoentry #price #buyersandsellers #productdifferential #swahili #economics #uchumi
Ramadhani Ausi Akili
 
Back
Top Bottom