Marekani yapeleka meli za kivita katika rasi ya Korea

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,369
8,072
Jeshi la Marekani limetoa amri kwa meli zake za kivita zinazobeba silaha zielekee karibu na rasi ya Korea, huku kukiwa na hofu kubwa kuhusiana na Korea Kaskazini kuimarisha silaha zake za kinukilia.

Msimamizi wa kijeshi wa Marekani wa eneo la Pacific alieleza kuwa kujiandaa huko kijeshi ni muhimu katika eneo hilo.

Meli hizo zinazojulikana kwa pamoja kama The Carl Vinson Strike Group zinashirikisha meli moja kubwa ya kubeba ndege za kivita na meli zingine za kivita za kawaida.



Awali ndege hizo zilitarajiwa kuzuru Australia lakini mkondo wake ukabadiliwa kuelekea Bahari ya Pacific.

Eneo hilo la Pacific ni kule ambako wanajeshi wa Marekani walifanya mazoezi ya kijeshi na wanamaji wa Korea Kusini.

Msemaji wa jeshi la Marekani anasema kuwa Korea Kaskazini ndilo tisho kubwa zaidi kwa usalama wa eneo la Pacific.



Anasema ushahidi ni jinsi taifa hilo linavyofanya mazoezi ya zana za kinukilia kiholela.
Mbali na kuwa na uwezo mkubwa wa kushambulia, meli hizo za kivita zina makombora yanayoweza kuzima zana zo zote zinazolengwa kwake.
 
Juzi Ijumaa Rais Trump alikuwa na mazungumzo mafupi na Rais wa China huko Florida. Haikufahamika mara moja mazungumzo yao yalihusu nini. A week earlier, US, Israel, na washirika wengine walionekana wakifanya mazoezi ya nguvu ku-penetrate various defense systems. Leo manowari za kivita zinaelekea kwa kasi rasi ya Korea. Mnyoa panki mwisho wake umekaribia ... Mrusi tayari "kashatiwa dl" kule Syria; katulia ...
 
Trumph ana asili ya kisukuma.. hajaribiw
Chini ya Trump uchumi wa Marekani utapaa sana. Utaweka historia ... Usalama pia utaimarika sana Marekani kuliko kipindi chochote cha watangulizi wake zaidi ya 50 yrs ago ... Demokrasia Marekani iko juu sana; mwananchi kumjibu Rais live ni jambo la kawaida sana. Transparency US ni ya hali ya juu sana; mmarekani mmoja ana thamani sana. Mahakama na Bunge viko huru sana katika kutekeleza majukumu yao hata kutengua amri za Rais ni kawaida sana ... na rais huheshimu maamuzi wala haweki vinyongo au visasi ...
 
Nakubali kwa kuwa wenzetu wana misingi ya uwazi ... thats why trumph ataifanya nchinkwenda mbele. Lakin kwa upande mwingine... nchi kama yakwetu... kuwa na rais wa aina hiyo... kwa uchum kama wa kwetu.. na aina ya siasa zetu.. nchi haitakuwa stable...
 
USA has a freedom to strike North Korea but not to that extent!!!!!

Hahahah eti "Not to that extent" hao hawatishwi kwa lugha hiyo sasa wana extension cable kubwa kinyama lakini Mkuu hujajificha sana hapo hahahahah inahitajika romanization
 
Yani Silla (Korea Kusini) Wanawashwa Sana Kila Na Wanawaogopa Sana Goguryeo (Korra Kaskazini).
 

Daaah kweli ulipitia kaole group Bagamoyo aisee bonge la mchepusho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…