Marekani yachunguza ajali ya gari linalojiendesha

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,249
160401145600_tesla_new_model_624x351_tesla.jpg
Image copyrightTESLA
Image captionTesla
Mamlaka ya Marekani inachunguza kifo cha kwanza kilichosababishwa na magari yanayojiendesha yenyewe.

Dereva wa gari la Tesla alifariki mjini Florida mnamo mwezi Mei baada ya kugongana na Lori.

Kinachochunguzwa ni progamu ya Auto Pilot ya Tesla ambayo hubadilisha mistari ya barabara na kujua iwapo kuna trafiki.

Katika taarifa,Tesla ilisema kuwa huenda gari hilo la S halikuweza kubaini upande mweupe wa lori hilo dhidi ya mbingu nyeupe iliokuwa ikionekana mbele yake

Kampuni hiyo imesema kuwa ajali hiyo ni hasara kubwa.

Ajali hiyo ilisababisha kifo cha dereva Joshua Brown mwenye umri wa miaka 40.

Dereva wa lori hilo hakujeruhiwa.

Marekani yachunguza ajali ya gari linalojiendesha - BBC Swahili
 
Back
Top Bottom