Nimesikia kuna watu (Watanzana wenzetu) wanawaita waandamanaji hawa cry babies au sore losers lakini kusema kweli Watanzania ni watu wa ajabu kweli kweli na nashindwa kabisa kuwaelewa. Maandamano kwa sasa yanafanyika Dunia nzima, toka London hadi Berlin, toka Sydney hadi Buenos Aires, toka Ottawa hadi Mexico City...labda ni Tanzania tu hatutashuhudia maandamano kwa sababu hatujui haki zetu.Sawa mkuu
Mambo yà siku mmoja tu. Weka akiba ya maneno yako.Naam, hiyo ndiyo demokrasia ya Marekani. Huwanyamazishi wapinzani wako baada ya kuapishwa kuwa Rais, mwisho wa uchaguzi ndio mwanzo wa harakati za kisiasa. Rais Obama, pamoja na ushindi wa kishindo, alianza kuonja joto la wahasimu wake toka siku ile ile anaapishwa.
Bahati ya Obama ni kwamba alikuwa na Wamarekani wengi nyuma yake. Donald Trump kwa upande wake Wamarekani wengi hawakumpigia kura ila kulingana na sheria walizojiwekea, anayepata kinachoitwa electoral votes ndiye hutangazwa mshindi.
Barack Obama akiapishwa mwaka 2009
Donald Trump akiapishwa mwaka 2017
Huko nyuma niliwahi kuonya kuwa Wamarekani kwa kuheshimu sheria na kanuni na kwa kuwa Donald Trump alishinda hawangeweza kuzuia asiapishwe. Lakini hiyo honeymoon yake ingeisha siku anakamata Kitabu takatifu na kula kiapo. Kwa kukubali kuapa huku alikjua yako mambo yanayohitaji maelezo amewapa wapinzani wake ruhusa rasmi ya kuanza mapambano.
Siku ya leo katika majimbo yote 50 ya Marekani kuna maandamano ya Wanawake dhidi ya Urais wa Donald Trump. Mjini Washington waliojitokeza na wanaoendelea kujitokeza kwenye maandamano ni maradufu ya waliojitokeza kwenye kuapishwa kwake. Hotuba yake aliyotoa jana imezidi kuwahamasisha wapinzani kuwa hatilii maanani tuhuma zinazoelekezwa kwake.
Hiyo ni miji miwili tu Washington DC na Chicago...na hii ni ya wanawake tu bado makundi mengine.
Wanawake wakiandamana mjini Washington.
Wanawake mjini Washington alikoapishwa Trump jana.
Wanawake wakiandamana mjini Chicago!
Kwa tuliokuwepo mwaka 1972 tunakumbuka jinsi Wamarekani walivyosubiri hadi Rais Richard Nixon ameapishwa kabla ya kuanza maandamano ya kumtoa. Somo kubwa hapa ni kwamba Donald Trump hawezi kuzuia haya maandamano na jaribio lolote la kufanya hivyo itakuwa ni sawa kumwaga petroli kwenye moto.
Tutaendelea kuwapa taarifa...
Ila waandamanaji wakae wakijua msemo usemao JOGOO AWIKE ,ASIWIKE KUTAKUCHA. WAMVUMILIE TU TRUMP
Huu msemo uko kwetu. Kuna mambo unaweza kulazimisha lkn mengine huwezi.
Hivi maandamano yakizidi yakimtaka aachie ngazi unadhani hataachia?
Utaongozaje watu wasiokuta uwaongoze?
Ubabe wowote ule una kikomo chake. Tuwaache wamarekani washughulike na Trump wao.
Mkuu mnaandamana kwakuwa Trump kamtukana Obama?Nimesikia kuna watu (Watanzana wenzetu) wanawaita waandamanaji hawa cry babies au sore losers lakini kusema kweli Watanzania ni watu wa ajabu kweli kweli na nashindwa kabisa kuwaelewa. Maandamano kwa sasa yanafanyika Dunia nzima, toka London hadi Berlin, toka Sydney hadi Buenos Aires, toka Ottawa hadi Mexico City...labda ni Tanzania tu hatutashuhudia maandamano kwa sababu hatujui haki zetu.
Donald Trump ni adui wa dunia na nina hakika nchi kama Marekani iliyopigania uhuru wake kwa kumwaga damu hawawezi kumkubali fashisti Trump! Trump amekuwa kimtukana Obama stupid bila kujali kuwa hamfikii Obama kwa IQ kubwa, amemtukana mpigania haki za binadamu John Lewis kwamba ni spent force...na hii yote ni kwa sababu ya uweusi wao lakini wapo Watanzania wenzetu wanashangilia.
Hawa wako nje ya jengo lake la Trump Tower wakimsubiri.
Huko askari polisi wanaendeshwa na akili zao sio zile za kushikiwa!!
Kwa wastaarabu kazi ya Polisi ni kusindikiza maandamano na si kupiga waandamanaji!
Sijui sisi Watanzania tuko karne ya ngapi!