Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,269
- 23,205
Naam, hiyo ndiyo demokrasia ya Marekani. Huwanyamazishi wapinzani wako baada ya kuapishwa kuwa Rais, mwisho wa uchaguzi ndio mwanzo wa harakati za kisiasa. Rais Obama, pamoja na ushindi wa kishindo, alianza kuonja joto la wahasimu wake toka siku ile ile anaapishwa.
Bahati ya Obama ni kwamba alikuwa na Wamarekani wengi nyuma yake. Donald Trump kwa upande wake Wamarekani wengi hawakumpigia kura ila kulingana na sheria walizojiwekea, anayepata kinachoitwa electoral votes ndiye hutangazwa mshindi.
Huko nyuma niliwahi kuonya kuwa Wamarekani kwa kuheshimu sheria na kanuni na kwa kuwa Donald Trump alishinda hawangeweza kuzuia asiapishwe. Lakini hiyo honeymoon yake ingeisha siku anakamata Kitabu takatifu na kula kiapo. Kwa kukubali kuapa huku alikjua yako mambo yanayohitaji maelezo amewapa wapinzani wake ruhusa rasmi ya kuanza mapambano.
Siku ya leo katika majimbo yote 50 ya Marekani kuna maandamano ya Wanawake dhidi ya Urais wa Donald Trump. Mjini Washington waliojitokeza na wanaoendelea kujitokeza kwenye maandamano ni maradufu ya waliojitokeza kwenye kuapishwa kwake. Hotuba yake aliyotoa jana imezidi kuwahamasisha wapinzani kuwa hatilii maanani tuhuma zinazoelekezwa kwake.
Wanawake wakiandamana mjini Washington.
Wanawake mjini Washington alikoapishwa Trump jana.
Wanawake wakiandamana mjini Chicago!
Hiyo ni miji miwili tu Washington DC na Chicago...na hii ni ya wanawake tu bado makundi mengine.
Kwa tuliokuwepo mwaka 1972 tunakumbuka jinsi Wamarekani walivyosubiri hadi Rais Richard Nixon ameapishwa kabla ya kuanza maandamano ya kumtoa. Somo kubwa hapa ni kwamba Donald Trump hawezi kuzuia haya maandamano na jaribio lolote la kufanya hivyo itakuwa ni sawa kumwaga petroli kwenye moto.
Tutaendelea kuwapa taarifa...