Uhuru, demokrasia na haki za binadamu ni mambo ya msingi wewe.......alichokifanya huyo dada ni kuvuka mipaka.
Sawa kama kuna na mipaka. Ila sijui ikoje hiyo mipaka yenyewe. Huyo kaonesha tu sanamu, Mtikila alimtukana kabisa Nyerere na akashinda mahakamani kwa kigezo cha uhuru wa kutoa maoni.
Nilichomaanisha, wanachotuhubiria na kututaka sisi tukiishi hata wao hawakiishi. Nimefurahi kusikia kila jambo lina mipaka, hata enzi ya Mwl. kulikuwa na hiyo mipaka pia, ila watu walitaka kujiachia zaidi.
Demokrasia ya Marekani kisiasa tumeishuhudia, haifati kanuni kuu ya kidemokrasia, "wengi wape au sauti ya wengi ni sauti ya Mungu" wateule wachache wanaweza badilisha sauti ya wengi.
Haki za binadamu, hadi leo Marekani ndo muharibuji mkuu ustawi wa mataifa mengine, kiuchumi, kijeshi, kisiasa nk. Hizo haki ni za binadamu au za wamarekani?
Uhuru, hapo tumejifunza kwamba una mipaka. Huku tukimfikisha maahakani mtu anayemsema raisi vibaya, au tukilifungia gazeti wanatupigia kelele, hiyo mipaka inajengwa na nani Kama si sisi wenyewe kulingana na sheria, tamaduni na ustaarabu wetu?