Marekani imeanza kuishiwa na mbinu za ujasusi?


mkui itapendeza ukifanya hivo
Nyinyi ni waumini wa conspiracy theories?

Maana kuamini masuala kama controlled demolitions, kwamba vilipuzi vilipandikizwa ndani ya majengo kabla ya tukio. Kwamba Marekani ilikuwa ikitafuta justification ya kuivamia Afghanistan n.k. inahitaji kuwa muumini haswa wa masuala hayo.

Wapo pia wanaoamini kuwa dunia ni kama sahani ya kulia ugali. Wote hao wamo katika kundi moja linalofahamika kama conspiracists.
 
mimi sipo upande wowote ila kutokana na sintofahamu mbalimbali.hasa kuhusiana na sept 11.binafsi nashindwa kuamini kabisa kama kweli OSAMA alihusika kwenye tukio lile.
na ndiomaana nahitaji kupata taarifa zaidi kwa wanaojua zaidi pengine kuna ambacho nitakiongezea kwa kile kidogo nilichokua nimepitia.
 
Bro nakuheshim sana. Please naomba ufute hii comment yako.
Kaandika urojo na huyu mshana jr bila shAka Ni mkongwe huju jf.
Naskitika mtu Kama huyu kusikiliza stori za kahawani na kutuletea.
Nb.
Mshana jr nyambizi Ni Ile huitwa submarine..
Ni kubwa Sana haiwezekani ikachimbiwa njia ya chini na ikatembea hasa kuekekea sehem nyeti kama bank
 
Saa kadhaa zilizopita, Joe Biden amesaini agizo kwa ajili ya uimarishwaji wa ulinzi katika masuala ya kimtandao (cybersecurity) ikiwa ni baada ya shambulio la kimtandao katika bomba la mafuta la Colonial.

Hiki ndicho nilichokisema hapo awali (post namba 7) kuhusu uboreshaji wa mbinu za kiusalama pale yanapotokea matishio mbalimbali ya kiusalama nikitolea mfano tukio la Septemba 11 na maboresho ya kiusalama yaliyofuatia baada ya shambulio lile.

1. CNBC | Biden signs executive order to strengthen U.S. cybersecurity defenses after Colonial Pipeline hack

2. Financial Times | Biden signs executive order to strengthen US cyber security

3. Reuters | Biden cybersecurity order mandates new rules for govt software
 
Hakuna mfumo wowote unaoendeshwa na na kompyuta ambao uko salama duniani. Kinachofanyika ni kuimarisha mbinu za kurecover control mapema zaid na kureverse engineer shambulio kuzuia kama hilo lisijirudie tena
 
Ila dunia ilifurahi sana Raisi Saddam Hussein kunyongwa adharani yaani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…