Kinau Michael
Member
- Aug 18, 2023
- 8
- 13
Je, Simba anaweza kumfunga AA Tripoli kwa Mkapa?
Simba SC Tanzania inarejea Lupasa kwa Mkapa ikiwa inahitaji ushindi ili kutinga hatua ya makundi michuao ya Klabu Bingwa Afrika huku wengi wakiwa na matumaini kuwa inaweza ikafanya hivyo bila ubishi kutokana na rekodi yake katika uwanja huo.
Timu nyingi kubwa zikija kucheza na Simba SC Tanzania zimekuwa zikishindwa kupata matokeo hapo na hiii ndio jeuri ya mashabiki wengi wa klabu hiyo kuelekea mchezo huo.
Ni wazi kuwa kuna makosa mengi yamefanya na Simba SC Tanzania wakiwa katika mechi yao ugenini hasa kupoteza nafasi walizotengeneza kipindi cha kwanza na muda mwingi kupoteza mipira (kukosa umakini), haya ni makosa ambayo hawapaswi kuyarudia mchezo ujao wakiwa nyumbani
Historia ya wao kufanya vizuri diba la nyumbani isiwe kigezo cha wao kubweteka na kuamini kuwa wanaweza kupita bila kufanyia marekebisho makosa waliyofanya kwani historia hiyo hiyo inaweza kuwahukumu kama ilivyokuwa hivyo kwa UD Songo waliopata sare na kusonga mbele.
Jwaneng Galaxy pia wamewahi kusitisha ndoto za Simba SC Tanzania dimba la Mkapa kwa kuwatandika bao tatu licha ya ushindi waliopata ugenini.
NI HAYO TU KWA SASA