MaRC na MaDC ujumbe wa Rais umewaingia?

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,345
Kauli ya Rais kwamba hajafanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa na wilaya kwa sababu alikuwa anawasoma kwanza utendaji wao wa kazi na mahusiano yao na wananchi ni ujumbe mzito sana uliotumwa kwa viongozi hao, nadhani mpaka kufikia kutamka hilo kishamaliza kazi.

Wale waliosema mtu yeyote atakayeugua kipindupindu akipona tu anapelekwa mahakamani ajiandae, aliyesema wazazi wa watoto wtakaofeli wacharazwe mboko naye akae mkao wa kung'oka.

Ila katika yote Rais asimuache kanali Fabian Massawe katika wakuu wake wa mikoa. Huyu alikuwa mchapa kazi aliyeondolewa kwa husda za wapinga maendeleo wa awamu ya JK. Massawe alikuwa mmoja wa maRc wachapakazi kwa vitendo.
 
Umetumwa na Massawe aisee si bure lkn kwa hili naamini wengi watatemwa maana wanafanya kwa kutaka waonekane kama wachapakazi lkn kiuhalisia ni sifuri
 

Massawe aliyeshindwa kumaliza mgogoro wa halmashauri ya Bukoba?! Au Massawe yupi huyo?
 
Massawe aliyeshindwa kumaliza mgogoro wa halmashauri ya Bukoba?! Au Massawe yupi huyo?
Mgogoro wa Halmashauri ya Bukoba ulikaa kisiasa na kimaslahi zaidi mpaka waziri mkuu na hata Rais walijihusisha nao. Na kazi ya RC si kutatua migogoro, kuna taratibu.
Sina uhusiano wowote na kanali wala hanijui mpaka anitume, nazungumzia utendaji wake.
 

Kama sio kazi ya RC kushughulikia migogoro kama huo wa Bukoba among many others; basi comrade hujui unachokizungumzia na kwa hiyo hukuwa na sababu ya kumpigia bigula kwamba ni mchapa kazi! Kwa kiasi kikubwa Massawe huyo ni mtu wa mizaha mizaha zaidi kuliko utendaji utafikiri alizaliwa pacha na Mkwere!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…