Fantastic Beast
Member
- Feb 18, 2019
- 52
- 537
Kuanzia kwa Mwinyi mpaka aliyepita Shein, sifa kubwa iliyowawezesha kuuwezea Urais wa JMT ni cha kwanza walikuwa humble na hawakuwa na skendo chafu chafu.
Kimsingi ili Rais kutoka visiwani aweze kutoboa kuiongoza JMT ni lazima asifanye maamuzi ambayo yatawafanya Watanganyika wajione kama wamekuja kuibiwa au kutawaliwa kimabavu na Mzanzibari.
Hii yote ni kwa sababu ya kuulinda muungano.
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar haukuwa Muungano wenye ridhaa ya wananchi ndiyo maana una maswali mengi kuliko majibu. Mwalimu Nyerere aliulinda Muungano huu kwa nguvu, akili zake. Ndiyo maana aliyeuhoji hakueleweka.
Siku chache baada ya Tanganyika kupata uhuru wake mwaka 1961, rais wa wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kukaririwa akijuta nchi yake kuwa karibu na Visiwa vya Zanzibar. Akiwa katika moja ya tafrija katika Ikulu ya Dar es Salaam, Mwalimu Nyerere alisema angekuwa na uwezo angevivuta Visiwa vya Zanzibar viungane na Tanganyika au angevisukuma mbali kabisa vipotee.
Mwalimu aliyasema hayo wakati tayari joto la siasa likiwa linachemka katikav isiwa hivyo tangu mwaka 1957. Wakati huo vyama vya Afro Shiraz Party, ZNP, Umma Party na ZPPP
vikichuana kwa kasi.
Mwalimu Nyerere aliiona Zanzibar ni tishio kwa utawala wake na hapo ndipo akaanza kutafuta dawa. Ndiyo maana mwaka 1964 baada ya mapinduzi ya Zanzibar yaliyokipa nafasi Chama cha ASP, Mwalimu Nyerere alimshauri Abeid Karume waunganishe nchi zao.
Mwalimu Nyerere aliulinda Muungano huo kwa nguvu, akili zake zote. Ndiyo maana aliyeuhoji hakueleweka. Mfano sote tunakumbuka aliyomkuta aliyekuwa Rais wa Zanzibar baada ya hayati Karume, Mzee Aboud Jumbe ambaye mwaka 1983 alipoteza cheo hicho kwa kuchokonoa Muungano.
Mwalimu Nyerere alikuwa mkali siyo tu kwenye Muungano, bali ndani ya CCM kwa ujumla. Haikushangaza mwaka 1988 alipowafukuza uanachama kina Maalim Seif (Seif Sharif Hamad) na wenzake. Na kilichomtokea aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, Mansour Yusuf Himid kwenye bunge la katiba mpya kutokana na maoni yake ya Muungano wa Serikali tatu kinyume na msimamo wa CCM, ni mwendelezo wa fikra zile za Mwalimu Nyerere.
Yaani, pamoja na Mwenyekiti wa CCM wakati huo, Jakaya Kikwete kutoa fursa kwa Watanzania kubadili katiba yao ambapo kila mtu; awe mwana CCM au mwanachama wa chama chochote au asiye na chama atoe maoni yake, bado wengine walizuiwa kufikiri tofauti na chama.
Huo ni ubabe ndani ya CCM unaotumika kuzima fikra mbadala za Watanzania si katika muungano tu, bali hata katika mustakabali wa maisha yao. Kwa CCM, suala la Muungano ni kidonda hasa inapotokea Wazanzibari wanadai uhuru wa nchi yao kamili. Ndiyo maana wanasisitiza Serikali mbili ili Serikali ya Muungano iendelee kuitawala ya Zanzibar.
Kila linalohusu utawala wa Zanzibar huamuliwa kwenye vikao vya CCM mjini Dodoma na ukitaka kutawala visiwa hivyo shurti uwapigie wao magoti.
Sababu kubwa ya Marais wa JMT kutoka Visiwani kutakiwa kuplay low key ni ili kuepusha maswali ya uhalali wa Muungano kutokea upande wa Tanganyika kwani ndiyo itakuwa mwisho wa JMT.
Kwa yanayoendelea sasa nchini katika medali ya siasa, kinafanya kile kidonda wa wazanzibari cha kudai uhuru wao kamili kihamie na kwa Watanganyika. Kitu ambacho waasisi wa nchi hizi mbili na Muungano walihakikisha hakitokei.
Hakika kwa sasa hakuna Mtanganyika anayemuelewa aliyekaa pale juu.
Swali ni JE, CCM WAMEAMUA KUKUBALI MUUNGANO UVUNJIKE KWA KUVUNJA MIIKO WALIYOIWEKA WAASISI WA TAIFA?
PIA SOMA
- Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?