Marais wa Afrika warudi kwenye nafasi zao Za Umwinyi

Indian

JF-Expert Member
Oct 27, 2012
821
708
Marais wa Afrika warudi kwenye nafasi zao Za Umwinyi

Si dharau, Ni ujumbe.
Nchi nyingi Za kiafrika Ni shahalabahala, Hazina mifumo iliyonyooka, Hazina miundombinu inayorizisha, Hazina matibabu, demokrasia n zero, Hazina elimu. Ukiangalia kwa mfano Tanzania vyanzo vingi vinavotumika sasa vimeachwa Na mkoloni. Na wakati huo mkoloni yupo kulikua Na matibabu bora, elimu Na miundombinu Mbinu mizuri iliyovutia hata Kama ilikua michache Na baadhi ya maeneo kutokana Na mahitaji ya watu.

Viongozi ambao Leo Ndio Marais wetu wamebaki kulalamika, Mara wakikabidhiwa ukubwa huu wanachanganyikiwa Na Hawajui Waanze Wapi Na wanatarajia kufikia Wapi?
Enzi zile waafrika walikua wakionekana wanaweza sana waliopokua wamepewa nafasi Za Umwinyi kila kata Na hii Ndio nafasi ya kiongozi wa Afrika ambazo Leo walitakiwa wawepo ili kuendeleza Nchi hizi.

Nina maana kubwa sana nikasema hivi Na matukio yanaonekana ndani ya Tz Na Bara la Afrika. Kuongoza Sio kutumia maneno makali,kejeli,Kebehi au kukomoa wengine, Ni misingi bora Maraisi wa Afrika Hawana Na wanapoelekezwa Ni ubishi Kama hii imekua Ndio Nembo ya muafrika.
Ukiangalia sasa utaambiwa maendeleo yanaonekana ya majumba tuu, Na barabara refu lkn kwa mwananchi wa kawaida Ni majonzi awe anafanya kazi au hafanyi kazi.

Tukikosa hili ninakuja Na hili:
Tukubali matokeo, tukubali kuwa hatuna upeo wa kuona mbali, tukijenga Leo kesho tunabomoa. Nashauri tuagize wataalamu waje watupangie, utawala,miundombinu,elimu,malighafi ambazo mpk Leo hazionekani zinaisadia nini Nchi. Tukikubali kupangiwa bila ya ubishi Ni kukubali kuachana Na 10pacent ambayo viongozi wengi Ndio inayosababisha kulipoteza Taifa kwenye muelekeo.

Hawa wazungu kwa wakati Sio uwape gesi,Sio uwape dhahabu, wape ofisi wasimamie Na kupanga kodi, Kama waingireza Ni wataalam sana wa kodi ukiwapa nafasi ya kutupangia kodi zetu hutomsikia mtu kulalamika.

Tukubali tumeshindwa Na ishara ya kushindwa imeshaonekana zaidi ya miaka 50 iliyopita Kwanini tusikubali?
 
Hapa ndio umefunga kazi! " Ukiangalia kwa mfano Tanzania vyanzo vingi vinavotumika sasa vimeachwa Na mkoloni. Na wakati huo mkoloni yupo kulikua Na matibabu bora, elimu Na miundombinu Mbinu mizuri iliyovutia hata Kama ilikua michache Na baadhi ya maeneo kutokana Na mahitaji ya watu." (mwisho wa kukunukuu) Naona unajiunga tena na mzee Sumaye na EL kwenye kampeni yao ya mwaka jana!
 
Unaweza kutaja hivyo vyanzo vingi tuone wingi wake?
 

Si vyema kutaja watu, ungeniuliza Swali lolote ningekujibu lkn matusi hayajengi, Na Hapa ndipo unapoziona akili Za muafrika zilipoishia.
 
Kwa wakati huu hutoviona, sasa ivi utaona uwanja wa Taifa Na Darja jipya tuu.
Ni vizuri ukataja ili kupanua mjadala, si watu wote wana uelewa ulionao. Sijabisha ninahitaji kufahamu zaidi
 
Si vyema kutaja watu, ungeniuliza Swali lolote ningekujibu lkn matusi hayajengi, Na Hapa ndipo unapoziona akili Za muafrika zilipoishia.
Kumbe wewe ni mzungu mwenye akili nzuri? Poor vijana wetu wa siku hizi! Unajidharau mwenyewe? Haingii akilini kabisa nafikiri haya ni matokeo ya maadili! Unataka kutuambia toka mkoloni ameondoka hamna jipya na zuri lililofanyika?
 
Kumbe wewe ni mzungu mwenye akili nzuri? Poor vijana wetu wa siku hizi! Unajidharau mwenyewe? Haingii akilini kabisa nafikiri haya ni matokeo ya maadili! Unataka kutuambia toka mkoloni ameondoka hamna jipya na zuri lililofanyika?

Jipya liko wapi? Dhulma, Rushwa, ukandamizaji, ubaguzi Na ukabila umeshika kasi, Na kwa kasi zaidi mnajificha kwakua Ni wakoloni weusi tuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…