Jabali la Siasa
JF-Expert Member
- Jul 10, 2020
- 2,682
- 2,344
Na Mwandishi Wetu, Serengeti
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulurhaman Kinana amepokea malalamiko mbalimbali yakiwemo madai ya mauaji ya wananchi katika hifadhi ya Serengeti mkoani Mara.
Amesisitiza kuwa hakuna mwenye haki ya kukatisha uhai wa mtu mwingine.
Akizungumza leo Mugumu, Serengeti mkoani Mara, aliposhiriki kikao Maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Serengeti, Kinana ameeleza kuwa ipo kwa viongozi kuendelea kuwaelimisha wananchi kuheshimu mipaka iliyopo.
“Mkuu wa wilaya ya Serengeti amelifafanua vizuri sana na huwezi kuulaumu upande mmoja peke yake, lakini tunawajibu wa kuwaelimisha wananchi kuhusu kuheshimu mipaka lakini jambo moja la msingi hakuna mwenye haki ya kuondoa uhai wa mtu. Hata katika Katiba haki ya kwanza ni kuishi,” amesema.
Kinana ameelezea hayo baada ya baadhi ya wana CCM akiwemo Diwani wa Kata ya Machochwe Joseph Magete kudai kuwa kumekuwepo na matukio ya kutatanisha pembezoni mwa hifadhi hiyo kwa watu kupotea, hivyo alimuomba Makamu Mwenyekiti kuliangalia suala hilo kwa nini linatokea katika maeneo hayo.
Kwa mujibu wa Kinana, serikali hairuhusu kundolewa maisha ya mwananchi yeyote na kwamba vyombo vya ulinzi na usalama wajibu wake ni kufuata sheria.
Hata hivyo, alisema katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto hiyo tayari serikali imeunda kamati ndogo ambayo itafika mkoani Mara kufanya tathimini na hatimaye kutatua changamoto hiyo.
== ==