Mapungufu ya Zawadi ya YERIKO ya Jumapili kwa Rais Mh John Pombe Magufuli

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Mods naomba msiunganishe huu uzi

Hongera kwa Kuandika vitu vyenye nia chanya juu ya changamoto ya nchi yetu.

ZIFUATAZO NI CHANGAMOTO/MAPUNGUFU NILIZOZIN G'AMUA KWENYE BANDIKO LAKO ZURI.
ZAWADI YA JUMAPILI KWA MH. RAIS JOHN POMBE MAGUFULI
Mambo mengi unayosema yako kihisia..

1:Una chuki na CCM, Sijui kama unachuki na CCM au wanaCCM baadhi, Maana CCM kama taasisi na Misingi yake Ikisimamiwa katika Default zake haina tatizo kabisa. Ni sawa Useme Unachuki na BIBILIA kwa Sababu wakristo ni waovu au ndio wamesababisha Matatizo. Kumbe inaweza kuwa ni Ukengeufu wa wakristo sio bibilia. Huo ndio uelewa wangu kuhusu CCM. Kipaumbele cha Rais ni VIWANDA na hajawahi kuhama naona Utekelezaji wa Majukumu yake unaita Vipaumbele.


2:Mikataba Mibovu, Tunalia watanzania kuwa Mikataba mibovu, Inatunyonya. Zote hizi ni hisia maana mikataba yenyewe Hatujaiona, Na ubovu wake au Uimara wake hatuujui pia Isipokuwa waliosign na wenye access nayo. Badala ya kulia Mikataba Mibovu kwa hisia, Moja Tumuache Rais ambae nadhani anaaccess nazo na anania chanya na taifa apitie ajue nini cha kufanya na kama ni mibovu au sio mibovu. Pili ili kuepuka kuhisi, Tumuombe Rais na Bunge letu Lipitishe Sheria ya Trasnparency au Partial Transparency ya Mikataba ya Rasilimali pendwa kama madini na Gesi. Hapo Tutakuwa tunalaumu based on facts. Sisi sio wa kwanza kwa mikataba ya aina hiyohttps://www.jamiiforums.com/threads/rais-magufuli-mikataba-yote-iwe-wazi-au-nusu-wazi-itapunguza-surprise-nyingi-kama-hiyo-ya-makontena.1224026/

3:Sina Uhakika wa Hizo asilimia za Madini/Ore grade kwa hiyo migodi unazitoa wapi maana geita, wana grade tofauti na ore yao ni tofauti(Oxide Ore), Buzwagi na Buly (Sulphide Ore) na grade zao zote zinatofautiana huku grade ya Buzwagi ikiwa ndio ya mwisho na ndogo. Hii ni kwa Mujibu wa geologists.

4:Basis ya Makadilio yako hadi ukafikia hizo tani za dhahabu(1/4 ya 50,000 tons) umeitolea wapi. Hapo napo panasindikizwa na hisia ya kwamba tunaibiwa. Hadi sasa Ukweli uliopo kabla hatujapata ukweli mpya au Taarifa ya wataalamu Maprof wa Rais ni kwamba. Kila kontena lina wastani wa mchanga tani 20-25, asilimia ya concentration ya dhahabu ni 0.02 -0.05 ambayo inasemekana kuwa ni kubwa kulinganisha na concentrate nyingi duniani na ndio maana wawekezaji wanasema hiyo inachangia karibu 90% ya mapato kutoka kwenye mauzo ya huo mchanga wote na sio Copper kama migodi mingine ya cupper. Hivyo basi utapata kila kontena lina wastani wa kilo 4 hadi 5, na ambayo kwa tan 50,0000 wenda ikawa 2Tons ambazo hupimwa kwa OUNCES. Sio kidogo ni mabillion ya pesa. Hizi ni kwa mujibu wa wawekezaji,Tume iliyowahi kuchunguza kuleta smelter hapa nchini, na watu wanaofanya hiyo kazi huko. Hadit tutakapopata taarifa mpya za Kiuchunchunguzi ndio tutafuta haya na kuweka elimu mpya based on facts and testings.

5: WAJENGE SMELTER WATATUKATA KWENYE Mrahaba? Mrahaba ulikuwa 3% na baadae tukauongeza 4% na mtambo ni wa mabilioni. Ni pesa kidogo mno ukisema watukate maana yake sisi ndio hata madini yatakuwa hayana faida kabisa. Inawezekana Kujenga Smelter yenye hiyo capacity watu wetu wakitafiti na kuja na majawabu kutoka huko dunia ya madini. Mimi pia Nampongeza RAIS kwa KUMTUMA CAG, Wwao wanasema Wataanza Kulipa Cooperate Income Tax baada ya Kutimiza pesa yao waliowekeza ambayo kwa mahesabu yao WATATIMIZA 2019, na ndio maana Juzijuzi walitoa Inadvance Cooperate Tax ambayo wanapaswa kulipa kuanzaia 2019. Wenda CGA akagundua wanatudanganya Wamesharudisha Pesa yao na Badala ya Kulipa Mrahaba 4% waanze Kulipa Cooperate Tax ambayo ni kama 30%. Hapo Tutaandamana Kumpongeza Rais maana hadi sasa anastahili pongezi.

6:Baada ya Katazo la Rais (ANASTAHILI PONGEZI NYINGI), Mambo mengi yamegundulika ambayo bila katazo tungeendelea kuwa Gizani. Kwanza Tutapata Ukweli pili Wawekezaji watajua Nchi hii sio ile walioingia wakiona kila kitu hata kama sio chema kinawezekana. Mfano Mule kuna Madini mengi zaidi ya Copper/Gold/Silver kitu ambacho kilikuwa hakieleweki sana. Tatizo linakuja wawekejazi wanasema ni kidogo sana, Tena hata wao sio mali yao. All byproducts inabaki kama mali ya Smelter. Kumbe wakijenga hapa badala ile kubaki mali ya mchina/Mjapani au Mjerumani inabaki hapa inakuwa processed hapa na tunapata faida. Hiyo kidogo hatupaswi kuambiwa ni kidogo tu bali Tukathibitishe hukohuko hata kama vipimo huku ni vinaonyesha ni kidogo, Na tudukue huyo smelter anafaidika vipi. Tukigundua anafaidi na Hatuna Uwezo wa kuijenga hapa. Tunayafufua nayo yote hata kama ni kumi yaingizwe kwenye mkokotoo wa kodi.
Changamoto hatujui Wawekezaji na huyo Mchenjuaji huko nje wanamkataba gani? Tuko gizani.

Mapendekezo.
1: Tulilie Transparency ya mikataba au angalau iende kwa wakilishi wetu, Hii itaondoa hisia nyingi ambazo wenda hazikuwa na sababu. Amani Itamuongezea Trust muwekezaji kwa jamii ya kimataifa na watu wanaomzunguka/Wananchi
2:Tutrain watu Competent kwenye mambo ya mikataba na Negotiation za kimataifa kama ulivyopendekeza.
3:Wawakilishi wetu wajitahidi kuwa na Taarifa sahihi juu ya mambo yanayoendelea katika maeneo yao, Kiongozi wa eneo husika hajui hata kama huwa kuna copper au kwa nini kuna mchanga buzwg/Buly na sio Geita. Unakuta mbunge jimbo linamgodi lakni anaongea vitu ambavyo inaonyesha Hajui chochote kinachoendelea kuhusu wawekezaji eneo lake. Sasa unategemea huyu atawalisha nini wananchi wake kama sio vitu vya kuhisi. Tujue normal operations ili tuwe na uwezo wa kuidentify abdnormal operations.

Mwisho naungana na Wewe Kumpongeza Rais kwa kuvalia njuga mambo makubwa yenye utata lakini yanafaida kwa masikini,wasio na ajira, walemavu,wajawazito wasio na zahanati. Hili hata kwenye record mbinguni litaingia na tutalielewa zaidi siku akiondoka.

mkulima mwenzako katika tafakuri shambani...,

Ninakubali kukosolewa,kupingwa,kusahihishwa,kukemewa,kupongeza au kurekebishwa katika maoni yangu juu ya bandiko lako...
CCYeriko Nyerere
 
Nimeona umeongeza kitu katika mjadala. umejadili kwa kutumia taaluma sio nadharia na stori za vijiwe vya kahawa...
Bravo mkuu
mkuu hii sio taaluma yangu, sisi wakulima tumejifunza kutoa elimu za vijiweni na kutafuta ambazo angalau zinakaribiana na ukweli kwa faida ya yoyote anaependa sio political edge...
 
Hoja ya kujenga smelter haitokani na dhahabu Kiasi gani, bali na gharama za usafiri na uchembuaji. Gharama za kusafirisha na kuchembua mchanga China, ni sawa na kujenga smelter Tanzania.

Achana na mawazo ya asilimia za dhahabu, Shaba na fedha. Jikite kwenye gharama za kusafirisha na kuchembua huko China na Japan.

Watu humu mnapoteza muda na rasilimali kwa hoja zisizo na tija, hata hiyo tume ya Maghufuli itaenda kupoteza muda kama haitafanya utafiti wa gharama za usafirishaji na upembuzi wa mchanga.
 
Safi imekaa vizur
 
Ghalama za Usafirishaji sio hoja na sio siri. Kwa sababu kwako ni hoja, tuelee angalau estimates na ulinganishe kilichomo kama ni ghalama za ajabu. Kama kwao ingekuwa ni ghalama wangeshaleta hiyo smelter hapa siku nyingi.

Kwa upande wa Muwekezaji: Yeye shida sio ghalama bali ni Ghalama ya kuweka huo mtambo na mtambo mwenza(Sulphuric acid Plant). Pili anaangalia Life of Mine, mfano mmoja Buzwagi unakaribia kufungwa huo mwingine utabaki na production kubwa ila sio sana.
Kwa upande wetu: Kuna madini mengine mule wenda yakaongeza tija yakisafishiwa hapa, Pili Tutaongeza Ajira, Tatu Tutajua fika kama kinachokadiliwa kupatikana huko ndicho chenyewe halisi, nne Yawezekana kinachosafirishwa kwa mujibu wa taarifa za muwekejazi na wakaguzi wa madini sio sahihi wenda kunaudanganyifu. Ndio maana Unaona Rais anatafuta Jibu la swali lililodumu Miaka mingi bila majibu na Tunampongeza bila hiana.
Pia Tunasema kama US walijenga Smelter 1999 mgodi wa Stillwater ambao ni kama hz wanazodai ni capacity ni kubwa sana na Wenzetu huo mgodi una Capacity ya 20,000Tons annually japo wao wanadili na Mabaki sio Cupper wala Gold maana mabaki yao ni Platnum etc na yanakiwango kikubwa, Inashindikana nini leo 2017 kuwepo na kitu kama hicho kwa ajili ya sisi wabongo huku ili tunufaike. Hapo ndipo tunapokwamia katika tafakuri za madini wakati tunasubiri majibu rasmi kutoka kwa wataalam
 
Bandiko limeshiba elimu, safi sana mkuu. Rada ambayo inaitwa "rada ya chenge" ilinunuliwa kwa shilingi bilioni 81 lakini kichekesho ni kwamba uwezo wake unaishia Ngerengere tu yaani eneo lote linalobakia halipo chini ya uangalizi wetu.

Kuna rada nne zinanunuliwa ambazo thamani yake sio zaidi ya shilingi bilioni 65 na zitaliweka anga lote la Tanzania katika uangalizi wa muda wote, sasa nisiulizwe kama "rada ya chenge" watu walipiga au hawakupiga.

Nimeziongelea rada nne kwa sababu ndege zinazokwenda migodini haswa pale Bulyanhulu hazionekani kwenye rada. Kila alhamisi ipo ndege ambayo inaingia bulyanhulu na kuondoka na mawe ya dhahabu. Tunaweza kujiuliza tu tangu jamaa waanze kuchimba dhahabu, zimeshapita alhamisi ngapi ambazo ndege zao zimeondoka na mali.

Kuvitetea vizazi vijavyo vya Tanzania ni kazi inayotakiwa kufanywa na kila mwenye elimu, uelewa na maono mema.
 
Hayo maelezo ya ndege kutoka na madini umeyatoa wapi mkuu, Maana ndio story za mitaani na watu wanaozunguka nje wasiojua hata nini kinaendelea humo ndani.
Uzalishaji wa Acacia tofauti na wachimbaji wasio Rasmi uko transparent kwa kiwango flani. Ushauri tafuta mtu yoyote anayefanya kazi humo ndani akueleze huwa mambo yanafanyikaje.
Kuhusu ndege kuondoka na Madini kama utaeleweshwa na TMAA,Wizara ya Madini au TRA(maana hao wanauwakilishi huko hadi tutakapogundua wandanganya au la lakni kumbuka michakato yote inafanywa na sisi watanzania tena tunakaa nao mitaani ), Au mtanzania mwenzako unaemuamini ni mzalendo na mkweli na yuko humo utajua hilo sio sawa.
Ili kuliweka sawa watu wa madini waliamua kuweka kipindi maalumu kuwaelezea wananchi kama wewe kujua nini huwa kiaendelea Iko youtube. Usikilize kisha ulinganishe na unachoelewa. Kuna chopper na Ngege ya kawaida na hazina uhusiano. Chopper ni kwa ajili ya Kusafirisha Madini na Ndege kule uwanjani ni abilia na haziendi popote zaidi ya Mwanza au DSM. Kama unaushahidi wa hayo ambayo yako nje ya utaratibu wao wa kawaida ambao uko wazi utueleze mkuu maana maarifa yote ni kwa faida yetu au Tume itatupa mwelekeo halisi.
 
Hoja yangu ni kuwa smelter ingejengwa Tanzania.

Gharama za kusafirisha ni 300$/tonne. Mgodi wa Bulyanhulu una life span ya 25yrs.
Tani za mchanga milioni moja kwa iaka 25 (40,000 tons/year).

Kusafirisha tani milioni moja ni dola milioni 300. Kuchembua tani milioni moja ni dola milioni 108. (108$/tonne).
Jumla ni dola milioni 400.

Hizo zingeweza kujenga smelter ndogo na kiwanda cha kukamata sulfuric acid.
 
Kaka mitale na midimu, mimi nimefanya kazi ya kuusafirisha huo mchanga pale Tanga Port kuanzia 2004 mpaka 2007. Kampuni niliyokuwa nafanyia kazi ndio iliyokuwa inafanya clearance ya huo mzigo.

Pia nilikuwa nakwenda bulyanhulu mara kwa mara kwa ajili ya kumshikia ofisi jamaa aliyekuwa pale akifanya kazi kwa ushirikiano na BGML, kazi yangu pia ilikuwa ni kuwaleta jamaa wa customs kwa ajili ya ufungaji wa seals. Nimeshaingia ndani ya process plant mara nyingi sana kwa ajili ya usimamizi wa kazi ya upakiaji wa mchanga kwenye makontena.

Ninapozungumzia ndege kuingia mgodini my friend I know what I'm talking about. Kila alhamisi hapo kwenye huo uwanja wa ndege nje ya mgodi, ndege maalum zinatua na gari maalum linaingia ndani ya process plant kwa ajili ya kuchukua dhahabu.

Ninaongelea kazi yangu ya zamani, siongelei mambo ambayo nimeyasikia kwenye kiti cha fundi viatu wa pale posta mpya.
 
Je hiyo dhahabu ilikuwa inachukuliwa kihalali au ilikuwa inaibiwa?
 
Sawa ila ngoja tuishie hapa kwa sasa, ila kama ungekuwa mdadisi kidogo na kuwauliza watu sahihi nini huwa kinafanyika na kama kuna uhusiano wowote kati ta ndege/chopper inayosafirisha madini(Officially under supervision ya gv officials) kwa maelezo yako kila alhamisi na ndege ya abilia Charter(Auric Air mara nyingi)/Dash 8(zamani) ambayo inabeba wafanyakazi wageni na contractors ungepata vitu vipya zaidi ya huo uzoefu wa kuingia process plant kupakia concentrates.
sitetei Muwekezaji ila natamani watu tujue normal ili tuwe na uwezo wa kulaumu abdnomals from normal.
Asante mkuu kwa uzoefu
 
Biashara yenye mkataba sio wizi. Kinachogomba ni nini kimeandikwa kwenye mkataba, na ni namna gani kinaweza kuwa na faida kwa pande zote husika.
nyongeza kidogo, na ikiwezekana mikataba ibadilishwe kama(wanaojua ni wao maana sisi tunasikia tu) inamapungufu ili tufaidi zaidi na sisi walalahoi
 
Dash 8 ni kwa ajili ya wafanyakazi, ilikuwa inakwenda mgodini mara mbili kwa wiki ikipakia watu pale katika uwanja wa ndege wa zamani.

Ndege inayobeba madini ni ndogo tu, inatua alhamisi mchana na kuondoka mchana huo huo.
 
mkuu hii sio taaluma yangu, sisi wakulima tumejifunza kutoa elimu za vijiweni na kutafuta ambazo angalau zinakaribiana na ukweli kwa faida ya yoyote anaependa sio political edge...
Poleni Sana Wakulima, Nasikia mmepewa 2.2% ya Bajeti ya mwaka mzima 2016/2017...

Kilimo kwanza ilikua Ni Propaganda.

hapa Ni AVIATION KWANZA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…