Wadau,
Jana nimeangalia mechi ya Taifa Stars na Lesotho na yafuatayo ndio niliyoyaona mimi kama mfuatiliaji soka wa mda mrefu.
1. Team haina ushirikiano yaani kila mchezaji anacheza kadiri anavyojua yeye hii ikapelekea kabisa kuonyesha jinsi baadhi ya wachezaji kama Samatta walivyotofauti kabisa na wachezaji wanaocheza ligi za ndani kwa mambo mengi kama jinsi ya kumiliki mpira, kutoa pasi e.t.c
2. Wachezaji kutokujua majukumu yao wanapokuwa uwanjani mfano Kichuya tofauti na kupiga kona sikujua jukumu lake uwanjani lilikuwa ni nini hakuonekana kabisa na wala mwalimu hakulitambua hilo
3. Wachezaji kuwa na papara wakati wakupokea mpira, wakati wa kutoa pasi na kadiri wanavyozidi kulisogelea lango la wapinzani (hili limekuwa tatizo la muda kidogo kwa timu nyingi za kiafrica, hili tatizo lilipungua saana kipindi cha Maximo naona sasa limerudi)
4. Japo pumzi wanayo lakini stamina ni tatizo jambo linalopelekea wachezaji wengi kuanguka anguka bila kuguswa
5. Mwalimu kufanya mabadilikio yasiyokuwa na tija. Sijui alilenga kufanya nini
6. Mwisho vijana vipaji wanavyo wanachotakiwa kupata ni mwelekezi sahihi. Yaani inatia hasira karibia kutoa machozi inapoonekana vipaji kama vile vinapotea kwa kutokuwa na waelekezi weledi(angalia Samatta anavyocheza kwa msisitizo)