Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 168
- 442
KAMPUNI ya Orano kutoka nchini Ufaransa imepata hasara kubwa kulingana na taarifa yake ya fedha ya nusu mwaka ( Januari hadi Juni 2024) iliyochapishwa na Yahoo Finance.
Taarifa hiyo inaonesha kwamba kampuni hiyo ilipata faida ya Euro Milioni 12 pekee ikilinganishwa na faida ya Euro Milioni 260 ambayo kampuni hiyo ilipata katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka 2023.
Kampuni hiyo iliyokuwa ikijihusisha na uchimbaji wa madini ya Uranium yaliyotumika kuzalisha umeme kwenye vinu vya Nyuklia vya nchini Ufaransa, ilipata hasara hiyo licha ya kwamba serikali ya kijeshi ya Niger ilikuwa haijawafutia leseni ya kuchimba madini nchini humo.
Hasara kubwa zaidi inatarajiwa katika ripoti ijayo ya fedha ya kuanzia Julai hadi Desemba 2024 kwani serikali ya Niger iliifutia kampuni hiyo leseni iliyoiruhusu kuchimba Uranium nchini Niger.
Kabla ya mapinduzi ya Niger yaliyotokea mwaka 2023 , Uranium ya nchini Niger ilikuwa ikitumiwa na nchi ya Ufaransa kuzalisha umeme kwa ajili ya mahitaji ya nchini humo pamoja na mauzo ya umeme nje ya nchi. Mwaka 2023 nchi ya Ufaransa iliongoza kwa mauzo ya umeme nje ya nchi kulinganisha na nchi nyingine
Zilizoko katika Umoja wa Ulaya. Mauzo ya umeme nje ya nchi yaliingizia nchi ya Ufaransa mabilioni ya dollar.
Chanzo: Yahoo Finance.