Mapenzi ya urozi/ndumba siyo mazuri epukana nayo

Nov 18, 2024
9
16
Kwema wana JF nawasalimia wote!

Niende moja Kwa moja kwenye mada, huu uzi nimeamua kuuleta ili kuwaonyesha ni jinsi gani mapenz ya urozi yalivyotaka kunisababishia uchizi au kuniondoa uhai kabisa.

Well! Ilikuwa mwaka 2016 chuoni mkoa x, nilikuwa mwaka wa kwanza mwaka huo.
Chuoni hapo nilifanikiwa kuingia katika mahusiano na Binti mmoja wa mkoani Tabora.
Tulipendana na hasa mimi nilimpenda sana, binti huyo tumuite Rozi.

Nilimpenda sana nayeye pia alionyesha kunipenda.
Mwaka wa pili mwishoni mambo yakaanza kubadilika nikaanza kuona mwenzangu kama mapenz yamepungua.
Nikaanza kufanya utafiti chini chini nikaanza kunusa vitu kama vile alikuwa ananisaliti na mtumishi wa umma sekta flani (siyo lecturer).

Nilikuja kuthibitisha Kwa kukuta sms wakichat mapenz live live.
Nilipomuuliza ndo nikawa kama vile nimeuwasha moto.
Hapo hapo akanambia hanitaki tena, nilishindwa kujikaza nilijiinamiq chini nikaona kama Dunia imenigeuzia mgongo nimebak pekeangu msituni.

Siku mbili zikapita hali yangu ikazidi kuwa mbaya, Rozi hatak kuniona na ameshadhamilia kuniacha.

CHANZO CHA MATATIZO YANGU.

Nilipatwa na wazo la kumtafuta mtaalamu ili anisaidia kumrudisha kwangu Rozi.
Kibaya zaidi sikuwa mtu wa kushea mambo yangu binafsi na watu wangu wa karibu pengine ningepata ushauri mzuri na nisingepatwa na shida yoyote.

Weekend ya wiki hiyo niliingia mtaani nikiwa na lengo la kumtafuta mtaalamu Kwa kisingizio kuwa kuna jamaa yangu anaumwa kama katupiwa majini kwahyo anahitaji mtaalamu wa kumsaidia.
Nilipata namba ya mtaalamu kupitia mshikaji flani ambaye naye siyo kwamba tulikuwa na ukaribu kihivo mpka ningeweza kumueleza hali halisi.

Nikamchek mtaalamu, huyo mtaalamu alikuwa mbali kiasi na sehem niliyokuepo mimi, it's like nauli ni buku 20 kwenda na kurudi.
Nilimuelezea na nikamwambia mimi ni mwanachuo, akanambia kazi yako inawezekana hata tukiwa mbali mbali.

Kanipa maelekezo nimtumia majina yangu na ya Rozi, nimtumie pesa ya njiwa wawili na 50k ya kazi.
Nikamtumia pesa ya njiwa na majina nikatuma, cha kushangaza nimetuma kama leo usiku kesho yake asubuhi naona Rozi kanichek anadai anataka tuonane nikasema poa.

Hiyo asubuhi nikakutana na Rozi akanambia yaishe nimsamehe hatorudia tena na bado ananipenda.
Nikawaza hivi ndo dawa tayar au kajirudi mwenyewe. Nikawaza kama ni dawa huyo MGANGA kafanya usiku? Nikasema hapana hizi ni akili zake mwenyewe Rozi.
Fasta nikamchek MGANGA nikamwambia aahirishe zoezi hiyo pesa atumie tu asinirudishie, MGANGA akasema hapana tufanye tu maana nishanunua njiwa asubuhi hii ndo nimeamkia huko kutafuta njiwa na ninao hapa na nishaanza kazi.

Nikaona so kesi nikamwambia aendelee, ebana eeeeeeeh!😭😭😭😭 urozi siyo kitu kizuri.

Imefika saa kumi na moja jini tumetoka chuo, mimi nilikuwa nakaa mtaani yeye hostel chuoni, nikaona simu ya Rozi, baby upo wapi nimekumiss nataka nije kwako.
Eh nikasema tayari dawa zimeshika, nikamwambia nipo geto.
Dk 5 nyingi naskia boda nje Rozi huyu hapa mapenzi ni kama yalikuwa yamejiupdate yani alirudi Kwa kasi ya 9G.

Wivu, muda wote anataka niwe naye na malalamiko mengi mara hunipendi, unanisaliti muda wote anakagua simu na kila siku anataka tufanye mapenzi.

Yule MGANGA kanichek, vipi mbona hunipi mrejesho na wakati naona hapa kila kitu kipo sawa mimi nikajibu kiunyonge nashukuru lakini sidhani kama nitaweza hali hii maana ni usumbufu siyo mapenz tena.
MGANGA kasema hiyo nishamaliza kijana na kutengua inahitaj pesa ndefu, hapa nikaona MGANGA kanigeuza mimi kuwa kitegauchumi chake.

Nikawa navumilia hvo hvo, lakini hali ilikuwa mbaya sana lawama, wivu ngono vilinichosha nikamchek MGANGA nikamuliza bei gani kutengua akasema laki2 na nusu nikamtumia.

Hapa ndo ikawa kama nimejiingiza kwenye matatizo rasmi.
MGANGA akanitumia dawa ya unga unga rangi ya ugoro ilikuwa na harufu flani (nilikuja kugundua baadae kwamba ulikuwa ni uchawi)
Kanipa maelekezo nichemshe maji ya vuguvugu ya kuoga then niweke kama vijiko viwili, kumbuka hii nilijua ni dawa Kwa ajili ya kutengua ile ndumba.

Akanielekeza wakati wa kujimwagia yalw maji ninuie huku najitaja majina yangu, akanielekeza jinsi ya kunuia.

NDUGU ZANGU HUU NDO ULIKUWA MWANZO WA SHIDA.
Sikujua kumbe nilikuwa najiroga mwenyewe.
Usiku nimelala, ilikuwa usiku mnene sana nikasikia mwili unasisimka na jasho linatoka jingi sana na siyo kawaida macho pia nilikuwa nimeyatoa siyo kawaida.

Nilianza kuhisi kuna vitu vjnaingia mwilini, ile hali iliniatua na baada ya hapo nikawa mtu wa tofauti kabisa tofauti kabisa kabisa.
Nilianza kupatwa na hofu isiyo kifani, wasiwasi, kichwa kikawa kizito, hasira za hovyo, mapigo ya moyo yakabadilika yakawa yanaenda kasi, nikawa nazungumza mwenyew kimoyo moyo mambo ya hovyo hovyo tu.

Hali iliendelea kuwa mbaya mpka wanafunzi wenzangu aadhi wakawa wananiuliza shida nini, muda huo Rozi tayari karudi kwenye akili yake mapenz yakawa ya kawaida tu na alivoniona nipo vile nimebadilika nimekuwa mkali, sijali, nimejitanga basi nayeye akajitenga mazima.

Ikabaki ni Me, Myself and I, nilisumbuka sana masomo yakawa magumu kwangu japo Mungu mkubwa sikuwahi kupata sup, carry wala kudisco ( hapa Mungu tu ndo alinisimamia)

Nilienda hivo hivo ki ugumu ugumu mpka nikamaliza chuo lakini yule MGANGA akawa bado ananitafuta ananiambia kama ninateseka nimwambie nikajiuliza anajuaje kaama nateseka kama siyo nia ovu alonayo juu yangu?? MGANGA nikamblock hakunipata tena, nilikuwa napata ndoto mbaya, napaa, napiga mzigo madem mpk nakitupa, natumbukia kwenye shimo refu, in short it was not well hata kidogo.

Nilipomaliza chuo nikarudi home, nimefika home wote wananishangaa maana nilikuwa sitamanik, nimekonda, naongea kwa kujichanganya mda mwingine, hasira zo hovyo.

Ilinibidi nifunguke ukweli Kwa mama mwanzo mwisho na nilifanya vile kwasabab mama yangu ni muelewa nilijua ni lazima nitapata msaada japo niliaibika pia.

Nilipelekwa kanisani nikaombewa majini yakatoka na from that time moo leo nipo vizuri tu na maisha mengine yanaendelea.

Waganga siyo wote ni wazuri na siyo wote ni wabaya na kujiepusha na hayo maudhi basi tuache kwenda kwa waganga.

Nimemaliza.
 
Back
Top Bottom