SoC03 Mapenzi katika kazi yanavyochochea uzembe na kutowajibika

Stories of Change - 2023 Competition

hassan yahaya

Member
Aug 27, 2022
35
37
Ndugu wasomaji, ni wazi kwamba mapenzi mahala pake ni moyoni, na upendo wa kweli haufichiki, mtu akipenda ni ngumu sana kujizuia kutoa upendeleo kwa ampendae. Ukiambiwa tu "nakupenda" mwili wote unasisimka. Mapenzi hujengwa kwa misingi imara sana ambayo ni ngumu sana kuilegeza, leo hi mapenzi ndio hupelekea kutokuwajibika kwa wafanyakazi wa serikalini na ofisi binafsi. Mhusika akipigiwa simu tu "hallo" alafu ikakata anashindwa kuhudumia watu wenye shida mpaka amsikilize mpenzi wake. Mapenzi yanapozidi sana mtu anakuwa yuko tayari aache kazi, au ahame alipo awe karibu na ampendae.

Hatukatazi watu kupendana ila wanatakiwa kuchunga mamlaka walizopewa na kutekeleza majukumu ipasavyo. Mapenzi yanayoharibu utendaji wa kazi hayakubaliki. Mfano mwalimu wa kawaida akawa na mapenzi na mkuu wa shule haikatazwi na wala hainashida ila shida ni inakuja anagomea kufundisha na kuhudhuria vikao kwasababu ni mpenzi wa mkuu wa shule. Askari wa kawaida kuwa na mapenzi na mkuu wa kituo haikatazwi na hakuna ubaya ila ubaya ni kufanya makosa kama kutohudhuria kazini na mengineyo akafu mpenzi wake akamtetea. Pia mfanya biashara kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mhusika wa TRA sio kosa ila kosa ni kukwepa kulipa kodi kwakuwa mpenzi wake ni mtu wa TRA.

"Nakupenda " ni neno jepesi sana ila ni zito kwa wapendanao kwa kweli.
Mapenzi baina ya wapendanao yasiharibu ufanisj wa kazi. Mfano mwalimu kuwakasirikiw wanafunzi, kuwa adhabu kali na kuwatungia mtihani mgumu kisa mwalimu kagombana na mpenzi wake haifai. Kuna siku nililetewa mitihani ya kufungia muhula nilipoipitia ile ya masomo ambayo ninayafundisha niliona kunamwalimu katunga mtihani mgumu sana lakini sikumwbia siku hiyo ila baada ya kufungua muhula wa pili nilipomuuliza alisema ule mtihani aliandika tu maswali kwasababu alikuwa hayuko sawa kutokana na kuachana na mke wake. Mapenzi yalioelekea wanafunzi kufeli. Wafanyakazi wenzangu eouka kuwa na mahusiano na mfanyakazi mwenzio kwani ipo siku utakuja kugombana na wafanyakazi wenzako. Atatokea mfanyakazi mmoja atamtania mkeo au mumeo nafsi itakuuma, ukikaa kimya kumhofia mpenzi wako mkiwa kazini unajinyima uhuru utajiona unabanwa. Wanawake, tunawapenda sana ila inapotokea siku mkakasirikiana basi kasirikianenj wenyewe hadira zako usije nazo kazini. Fikiria, ikiwa umegombana na mpenzi wako hadi mkaachana alafu anakuja mfanyakazi mwenzio anaanza mahusiano naye je, utachukulia kawaida? haitokuuma, utaendelea kuongea nao? mapenzi acha yaitwe mapenzi tu, mkuu wa idara anakuwa mpenzi wa aliyekuwa mpenzi wako je, mtafanya kazi kwa pamoja? au kila mtu atafanya mambo yaje? utamsikiliza atakachokwambia?.

Mapenzi ni jambo nyeti sana katika jamii ila watu wanalichukulia kawaida tu. fikiria uzito wake, mtu ananunua gari la milioni mia nne anakuwekea na mafuta alafu anakuruhusu uende nalo safari yako lakini kamwe hawezi kukupa mpenzi wake ukalale bae hata kama kamuoa kwa elfu hamsini. Mapenzi ni hisia na hisia za mapenzi ni kali sana. Mapenzi yamegawanyika yapo yale ya asili mfano kati ya nama na mtoto, lakini pia yapo yasiyo ya asili mfano mke na mume. Mapenzi ya asili hayana shida sana ila shida ipo kubwa kwa haya yasiyo ya asili.

Mtu anaamka asubuhi anaacha kumjulia hali mzazi wake anampigia kwanza mpenzi wake. Vipi kazi ataifanya vizuri kama mpenzi wake hayuko sawa. Wahenga walisema ukipenda sana unakuwa chizi, uchizi uliosemwa hapa sio ule wa kuokota makopo ila ni ule kwa kumuwaza umpendaye kila wakati. Wafanyakazi huacha ofisi zao na kwenda kwa wapenzi wao ili kufurahisha nyoyo zao. Napenda kuwashauri walio kazini unatakiwa kutenga muda wako mda wa kazi fanya majukumu ya kazi, baada ya hapo ruksa kufanya unalolitakw kwa mpenzi wako.

Heshimu kazi uliyonayo, kama unafanya kazi TRA acha kumtetea mpenzi wako mwambie alipe kodi au mlipie. Wafanyakazi waliopewa ofisi, shughulikia watu kama utaratibu ulivyowekewa mpenzi wako naye asubiri kwani kila mtu anashida na wewe, usisite kumwambia umebanwa ba kazi anapokuhutaji mda wa kazi. Pia kama hakuna ulazima wa kuanzisha mahusiano na mfanyakazi mwenzio acha.

Mfanyakazi fanya tathmini ya mapenzi yako kama mnapoelekea ni salama na sahihi. Mapenzi yananguvh sana na nguvu yake ni ya kimwili yaani ni ngumu sana kuiepuka ila unaweza ukaihimili. Nawashauri kubadilisha mienendo katika kazi kwa kuiheshimu kazi na kutenga muda kwa ukitenga muda kila kitu kitaenda sawa. Mapenzi ni hisia na hisia mahali pake moyoni na moyo hubeba hisia kali za ila tuchunge hisia zetu.
 
Kfcoz ni tatizo na mbaya zaidi bado hatujajua nini haswa kimefichwa kwenye de liboloz na mbususu kiasi cha kwamba watu wakiunga isha tuu heshima hupungua
ila ni vyema kuchunga mazingira ya kazi kama mapenzi yawe nje ya kazi
 
Back
Top Bottom