Michael Amon
JF-Expert Member
- Dec 22, 2008
- 8,768
- 3,622
Wakuu,
Kwanza kabisa ninapenda kuchukua nafasi hii kuipongeza serikali kwa kusambaza mkongo wa Taifa wenye urefu wa 7,650 km ambao mpaka sasa umefika ambao umefika kwenye mikoa yote na kwenye makao makuu ya wilaya zote nchini Tanzania.
Pia ninapenda kuchukua nafasi hii kuishukuru serikali kwa kuruhusu makampuni ya SEACOM na Essay submarine cables kuja kuwekeza mikongo ya Taifa nchini Tanzania.
Hatua hizo zilizochukuliwa na serikali zimechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama ya mtandao wa internet na kuongeza ubora na kasi ya matumizi ya internet na data.
Lakini pamoja na jitihada hizo zilizofanywa na serikali, nasikitika kusema kuwa bado gharama za matumizi ya mtandano wa internet hali inayopeleke watu wengi kutumia internet yenye kasi ndogo kutokana na kiwango kikubwa cha bei ya kununua internet na mpaka sasa tumeshindwa kufikia hata wastani wa kasi internet ya dunia ya 5.1 Mbps, ambayo kama unapakua (download) file lenye ukubwa wa 1 GB itakuchukua dakika 25 tu kuweza kupakua file hilo.
Kutokana na hali hiyo napendekeza serikali ifanye yafuatayo ili gharama za internet ziweze kupungua lakini pia tuweze kuwa internet yenye kasi:
Serikali ipunguze gharama za kusafirisha bandwidth kwa kutumia mkongo wa Taifa
Uti wa mgongo wa internet (backbone) upo Dar es Salaam na ili internet hiyo iweze kufika mikoani na sehemu nyingi nchini lazima internet hiyo isafirishwe kwa kutumia mongo wa Taifa (National Fiber Optic Cable) ambapo serikali hutoza gharama kubwa kwa kampuni yoyote inayotoa huduma ya internet kusafirisha bandwidth yake kutoa eneo moja kwenda eneo jingine. Mfano: Kusafirisha bandwidth kutoka Dar hadi Arusha serikali inatoza $120 kwa 1 Mbps ambapo nadhani bei hii inaweza kuongezeka kadiri umbali unavyozidi kuongezeka.
Gharama hiyo ni kubwa sana uklinganisha na gharama ya kununua bandwidth kwa kwa hawa wawekezaji wa mkongo wa Taifa wa chini ya bahari ambao wao hutoza $80 kwa 1 Mbps. Ukiangalia hapa unaweza kuona jinsi gani serikali inavyochangia kufanya gharama za internet kuwa juu. Hivyo ninaiomba serikali iweze kupitia upya gharama hizo na kuangalia namna ya kuzipunguza gharama hizo.
Serikali ishawishi makampuni makubwa ya ISP kutoka nje kuja kuwekeza huduma ya internet Tanzania.
Ili kupunguza gharama za internet na kuongeza kasi ya matumizi ya internet pia ningependa kuishauri serikali ishawishi makampuni yanayotoa huduma ya internet kutoka nje yaje yawekeze huduma hiyo hapa nchini na hapa ningependa kupendekeza nchi ya Japan, South Korea na (Hong Kong) China hasa kwa sababu ya mahusiano mazuri ambayo tumeyejenga na nchi hizo kwa muda mrefu lakini pia kwa sababu nchi hizo ndio top 3 countries zinazoongoza kwa kuwa na internet yenye kasi na ya bei nafuu duniani.
Tukianza na Japan, hii ni nchi ya 3 inayoongoza kwa kuwa internet yenye kasi zaidi duniani ambapo watumiaji wa internet kutoka nchi hii wanapata internet yenye kasi ya wastani wa 15 Mbps hadi 78.4 Mbps. Kwa 15 Mbps kama unapakua (download) file lenye ukubwa wa 1 GB itakuchukua dakika 8 tu kuweza kupakua file hilo. Katika nchi hii internet yenye kasi ya 15 Mbps inauzwa kwa wastani wa $6 tu kwa mwezi.
Hong Kong, China ni nchi ya 2 inayoongoza kwa kuwa internet yenye kasi zaidi duniani ambapo watumiaji wa internet kutoka nchi hii wanapata internet yenye kasi ya wastani wa 15.8 Mbps hadi 101.1 Mbps. Kwa 15 Mbps kama unapakua (download) file lenye ukubwa wa 1 GB itakuchukua dakika 8 tu kuweza kupakua file hilo. Katika nchi hii internet yenye kasi ya 15.8 Mbps inauzwa kwa wastani wa $2.5 tu kwa mwezi.
Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, South Korea ndio nchi ni nchi ya 1 inayoongoza kwa kuwa internet yenye kasi zaidi duniani ambapo watumiaji wa internet kutoka nchi hii wanapata internet yenye kasi ya wastani wa 20.5 Mbps hadi 86.6 Mbps. Kwa 20.5 Mbps kama unapakua (download) file lenye ukubwa wa 1 GB itakuchukua dakika 6 tu kuweza kupakua file hilo. Katika nchi hii internet yenye kasi ya 15.8 Mbps inauzwa kwa wastani wa $2 tu kwa mwezi.
Ukitizama takwimu hizo unaweza kuona jinsi gani nchi hizo zinatoa huduma ya internet yenye kasi zaidi duniani na kwa bei nafuu. Hivyo kama tukifanikiwa kushawishi nchi hizo kuja kuwekeza Tanzania basi gharama ya internet itashuka kwa kiwango kikubwa sana na wananchi wengi wataweza kutumia internet yenye kasi kwa bei nafuu.
Nakaribisha mawazo yenu wadau na wazalendo wa nchi yetu juu ya namna ambavyo tunaweza kupunguza gharama na kuongeza kasi ya internet nchini.
Cc: Chief-Mkwawa, Kang, NingaR, Mwl.RCT, LEGE, leh