Mtoa hoja amejiweka katika kundi la watanzania wanaoipenda nchi yetu! Imekuwa ni jambo la kawaida kumsikia afande Sirro akitaja mapato lakini sijamsikia akitaja matumizi! Hapa panakuwa sio sawa! Fikiria mapato haya kandamizi kwa dsm pekee kwa siku nane pekee yanafikia million 600! 0.6 bilion je? kwa mwexi wote January itakuwa shilling ngapi? Kwa hesabu za haraka ni zaidi ya billion mbili! Sasa mbona matumizi yake yamekuwa siri kuu!
Kuna mengi yanaweza kufanywa ni hii michango ya tozo, moja likiwa na uboreshaji wa alama za usalama barabarani! Fikiria unakuta kibao cha speed limit kimezibwa na miti au hata kimegongwa na kuanguka chini hakionekani na unalazimishwa kwa nini hukuheshimu alama! Ninapendekeza hivi vibao ili kuleta attention viwekwe juu ya barabara across! Vikiwa na ishara nyingi kuashiria hatari! Jingine la muhimu ni kwa ndugu zangu askari kushauriana na wajenzi tanroads kuhusu umuhimu wa kuweka njia za waenda kwa miguu! Ni jambo la aibu sana unakuta manispaa au tanroads wanajenga barabara na hawafikirii kuweka njia ya waenda kwa miguu! Hii ni hatari sana Fikiria hizi barabara unakuta recently zimejengwa na hawa tanroads hawaoni umuhimu wa kuweka pedestrian way! Mifano ipo mingi kama barabara xote za manispaa, barabara nyingi za tanroads, mifano ni external kisukuru, Goba, mwenge morocco, mifano ipo mingi na zote haziakisi ukuaji endelevu wa jiji! Njia za waenda kwa miguu ni muhimu tanroads mnatakiwa mjiongeze! Mnapokwenda Japan study tour mnafikiri ni kupiga selfie tuu?