Uchaguzi 2025 Maoni yangu kwa kamati ya bunge kuhusu UBUNGE juu ya miswaada ya sheria za uchaguzi inayopendekezwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
46,721
66,981
1. Wabunge wote wachaguliwe kupitia kura za wananchi katika majimbo. Kusiwepo na wabunge wa viti maalum au wa kuteuliwa.

2. Jimbo moja la ubunge liundwe na idadi ya raia kati ya 150,000 hadi 160,000 na liwakilishwe na mbunge mmoja tu.

3. Mbunge aliyechaguliwa anapohama chama chake miaka miwili kabla ya uchaguzi mwingine chama chake kiteue mtu mwingine kuchukua ubunge wa jimbo husika.
 
Mimi nadhani bunge lisizidi watu 120. Yaani kila mbunge awe na jimbo la kama watu laki tano. Hii ni kumpuza gharama za wengi ambao hawana faida.

Pili ikiwezekana ni kuruhu wangombeaji pekee wasio na vyama hawa watasaidia kuweka uwiano kwa hoja badala ya kusopoti hoja za vyama hata jama hazina maslahi kwa taifa
 
Nje ya mada

pia posho na mishahara ya wabunge ipunguzwe maana ni mzigo kwa nchi .. hapo tutapata wawakilishi wa kweli sio wachumia tumbo
 
Mbunge asipoishi kwenye jimbo lake bila sababu ya msingi zaidi ya mwezi mmoja anakuwa amejivua ubunge.

Mbunge anaetetea serikali bungeni anakuwa amejivua ubunge! hakuna urafiki wa bunge na executive kwenye mambo ya wananchi.
 
Na pia ongezea hapo...
1. Uwizi wa kura, au kuharibu uchaguzi au matokeo ya uchaguzi iwe ni kosa la uhaini. Hii ni kwa sababu kuharibu uchanguzi ni sawa na kuweka uongozi usio halal kwenye nchi ambalo ni sawa na uhaini kabisa.
 
Mbunge anaetetea serikali bungeni anakuwa amejivua ubunge! hakuna urafiki wa bunge na executive kwenye mambo ya wananchi.
Dawa ya hii ni kuwa na wabunge binafsi... ambao tutakuwa na uhakika hawatadhibitiwa na chama Chao ila wawe wanazingatia maslahi ya wananchi.
 
Na pia ongezea hapo...
1. Uwizi wa kura, au kuharibu uchaguzi au matokeo ya uchaguzi iwe ni kosa la uhaini. Hii ni kwa sababu kuharibu uchanguzi ni sawa na kuweka uongozi usio halal kwenye nchi ambalo ni sawa na uhaini kabisa.
Sahihi kabisa
 
Mimi napendekeza bunge lisiwepo kabisa, maana mpaka sasa halijawahi kuwa na maana yoyote kimsingi.
 
Back
Top Bottom