Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,502
- 22,355
Nipo Dar-es-salaama kikazi na nimetua mitaa yangu ya katikati ya mji na nikamkumbuka msafisha viatu na maoni yake hatari ya kisiasa.
Nikakumbuka yupo mtaa wa Jamhuri lakini nilipofika pale sikumwona nikauliza mazee walokuwepo pale wakanambia kahamia mtaa wa Tandamti.
Basi kwa kuwa nilikuwa pia nataka niingie mitaa ya Kariakoo na nikakumbuka ninayo namba yake ya simu ambayo alinipatia (huwa napenda kuweka contacts za vyanzo vyangu vya habari) nikampigia.
Akanambia yupo mtaa wa Tandamti tangu mwezi wa December alipata kasehemu ka kujishikiza baada ya mjamaa aliekuwepo pale kuhamia sehemu ingine.
Basi, nikamfahamisha kwamba nikimaliza shughuli zangu pale Kariakoo ntamtafuta ili tujadili mawili matatu likiwemo suala la uchaguzi jinsi ulivyokwenda na nini ni maoni yake.
Baada ya mizunguko yangu nikaelekea mtaa wa Tandamti na pale nikamkuta anapiga kazi yake na ana wateja wapatao sita na kumbe tayari wana kikao chaendelea.
Pembeni yao alikuwepo kijana anakoka mkaa kwa ajili ya kahawa na kashata na upande mwingine alikuweo mzee mmoja ambae niliambiwa kuwa aitwa mzee Uledi mzee mashuhuri mahali pale kwa kuuza machungwa, mihogo ya kuchoma maji ya madafu na juisi maarufu ya miwa.
Hivyo hicho kilikuwa ni kijiwe tosha kabisa kuleta hamasa ya mijadala na mjadala nilioukuta ulikuwa ni wa kuhusu ugumu wa watanzania wengi wenye dhamana mbalimbali ambao wanapaswa kumsaidia raisi Magufuli na serikali yake katika kutekeleza azma ya serikali katika kuleta maendeleo ya kweli kwa watanzania.
Nikamwona mzee mwingine mstaafu aitwae Kigosi ambae nae ni wa "Tanga Line" alikuwa ile mitaa ya Jamhuri na msafisha viatu na nikashangaa kumwona pale.
Mzee Kigosi akaendelea kusema kwamba, "viongozi wengi hawana nia ya kweli ya kumsaidia huyu mzee. Wao wanangojea aondoke kwa matarajio kwamba raisi ajae atakuwa si kama huyu mwamba".
Akaendelea, " Wewe ona kila siku wasikia kuna madudu mengi yanaibuka watu wanapiga fedha nyingi zingine ni mabilioni kwenye miradi midogo tu. Watanzania wengi walizoea kutofanya kazi na kupenda maisha ya mkato, sasa wanapata taabu kwani amebana mirija hiyo".
Nikamuuliza mshona viatu kuhusu matokeo ya uchaguzi na nikampongeza kwa maono yake kwamba Tundu Lissu angeshindwa vibaya.
Mshona viatu akaendelea" Tundu Lissu ndio tegemeo la wazungu na ndio maana walihakikisha anaondoka salama Tanzania ili kwenda huko Ubelgiji kujiandaa na uchaguzi wa 2025."
Akaendelea. "wanadhani watakuwa na nafasi ingine tena ya kushinda uchaguzi ule lakini hiyo haiwezekani kwani CCM kwa sasa ndo imejizatiti kisawasawa".
Nikachomokea jina la Membe, mshona viatu akaendelea , " si umeona eeh Membe kamaliza kazi yake na yule mzee Maalim na Zitto nao wamemaliza kazi zao?"
Mshona viatu akaendelea, " kazi ya system ni kusoma mchezo na kuandaa kazi na mipango madhubuti na kama nilivyosema na waweza sema chochote lakini kwa sasa hali hali ndivyo ilivyo."
Nikamuuliza mzee Kigosi vipi anadhani ni nini serikali hii ifanye ili kuweka mambo sawa maana viongozi wengi waliopo wanaonekana wanafanya kazi kwa kutokujiamini.
Mzee Kigosi akaendelea " Raisi awape uhuru awape semina za kila mara na assurances kwamba wao ni viongozi alowaamini.
Awape miongozo kwani wengi ni vijana hivyo wana udhaifu wa kiujana ila wengi kama Bashe na Bashungwa na hata Jaffo ni viongozi makini wajao huko mbele."
Jamaa mwingine ambae alikuwa amekaa pembeni anasikiliza akaingia kutoa neno akaendelea kwamba, "JK ndie alieharibu sana hii nchi kwa miaka 10 mfululilizo na kulea taifa ambalo baadae linakuja kusumbua serikali zinazofuata."
Akaendelea, jamaa aliachia sana kila kitu na watu wengine hawakuzoea kujitafutia vipato kwa njia halali, wauza unga wengi, wakwepa kodi wengi, shule nyingi za "private" zilishamiri kuwakamua wananchi wa kawaida kwa kuondoa resources kwenye shule za serikali na kuziacha zibomoke na rasilimali za nchi kuibiwa bila Tanzania kufaidika na rasilimali hizo."
Mshona viatu akaendelea " Mji kama wa Dar wapaswa kusafishwa, ujengwe mazingira mazuri, mpangilio wa mitaa na maduka na wachuuzi wa barabarani waondolewe".
Akaendeelea, " pamoja na kwamba hawa pia ni walipa kodi lakini ni lazima waaandaliwe utaratibu mzuri wa kuuza bidhaa zao badala ya wanavyofanya sasa".
Mimi nikaangalia muda nikaona niwahi kuondoka kuelekea nyumbani Tegeta.
Nikatafakari yale niliyoyasikia lakini kikaguswa na hili la kwamba JK aliharibu sana hii nchi kwa miaka 10.
Nikajaribu kuoanisha miaka yake 10 na miaka 10 ijayo na JPM nikasema kimoyomoyo heru fikiria tungekuwa na miaka 20 ya "Hapa Kazi Tu" ingekuwaje?
Yalopita si ndwele tugange yajayo na nimeona mahala humu JF JK ataka kuandika (narudia kuandika) kitabu cha maisha yake.
JK aandike tu kitabu asijiulize ama aandike ama vipi.
JK aliingia serikalini kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 44 kijana mdogo, hivyo hayati baba wa taifa Mwalimu Nyerere alikuwa na matarajio yaani "expectations" kubwa juu ya JK.
Nikaangalia salio la charge kwenye simu yangu ili kuona kama naweza kuandika machache niliojifunza kutoka kwenye hichi kijiwe.
Hivi sasa nchi ipo kwenye kipindi kigumu sana serikali iko makini kutoza ushuru na kuhimiza wananchi kulipa kodi na kudai risiti.
Lakini pia serikali yapaswa kuangalia namna ya kutengeneza njia mbalimbali za kujipatia mapato zaidi.
Kwa mfano wakurugenzi wa halmashauri ni watu wa kwanza kabisa kuanza kufikiria kujipatia mapato katika halmashauri zao.
Halmashauri zaweza kuanzisha ushirikiano au "partnership" kati yao na wafanyabiashara waishio katika halmashauri hizo au hata wa kutoka nje ya halmashauri hizo na wawekezaji wa ndani na wa nje.
Kwa njia hii, halmashauri zaweza kuwa na "city centers" yaani katikati ya mji kunakuwa na maduka, maegesho ya magari, majengo ya kukodi kwa ajili ya ofisi, majengo ya maduka au "shopping malls", vivutio vya utalii wa ndani, viburudisho kwa ajili ya familia na watoto, mitaa maalum na maduka ya kawaida.
Pia wafanya biashara au wafanyabiashara watarajiwa wanaweza kushawishiwa kujenga maduka makubwa yaani supermarkets katika vitongoji vya halmashauri hizo hivyo kuweza kuketa mapato katika maeneo hayo kupitia kutoa ajira na kuwezesha huduma zingine kujitokeza katika maeneo hayo.
Kwa kuanzia njia hii yaweza kuzipatia mapato halmashauri nyingi tu nchini kiasi cha kuweka kupunguza fedha za miradi ya maendeleo ambazo zatokea serikali kuu na kuwa ni kiasi kidogo.
Njia ya pili kwa halmashauri kuweza kuongeza mapato katika maeneo yao ni kuhakikisha kila mwananchi analipa kodi ya maendeleo na kodi ya kiwanja kwa kuwa na utaratibu wa kusajili kila kiwanja na kila nyumba.
Ukiondoa misamaha ya kodi kila mtanzania ni lazima alipe kodi ili kulata maendeleo katika maeneo yao iwe ujenzi wa shule, barabara zinazopitika kwa urahisi.
Leo hii mtoto wa shule akichaguliwa kwenda sekondari ya kata ishakuwa taabu kwani kuna njia zingine magari hupata shida kupita kutokana na ubovu wa njia au vibarabara.
Hali hii italeta ugumu wa kuishi katika baadhi ya miji na vitongoji kwani watabakia wale wenye uwezo wa kuishi maeneo hayo na wale waso na uwezo kuhamia maeneo wanayostahiki.
Raisi Magufuli ana lengo zuri ila aina ya viongozi alio nao baadhi yao hawako tayari kufuata anayotaka.
Wapo baadhi Bashe, Bashungwa, Waziri mkuu Majaliwa, Lukuvi, Jaffo, na sasa Dr Gwajima na baadhi ya manaibu waziri wanaonyesha kuunga mkono maono ya raisi JPM.
Hajachelewa, asietaka kutumikia wananchi ajiondoe na apishe wenye nia hiyo ili maendeleo tunayohitaji wananchi yatufkie kwa uharaka.
Kila waziri na kiongozi khasa wale wanaowakilisha mikoani kama wakuu wa mikoa hadi wakurugenzi wa maendeleo ni lazima aunge mkono jitihada na juhudi za serikali.
Viongozi wachemshe vichwa wawe wabunifu wasiogope kutetea maamuzi yao endapo yanaleta tija.
Ni kama vile wanangojea muda wake uishe ili aondoke na kisha waendeleze ule ujinga wetu watanzania!
Kuwajibika katika nafasi aliyo nayo mtu ndio iwe mbiu ya kuchochea maendeleo kwa kila mtanzania.
Nimemaliza kuandika ndo nafika hapa Tegeta naenda kuicharge simu yangu maana yaelekea kuzima.
Wasalaam wanaJF.