Maoni kuhusu Ukatili wa Kijinsia kwa Watoto

RIGHT MARKER

Member
Apr 30, 2018
99
360
📖Mhadhara (61)✍️
MAONI KUHUSU UKATILI WA KIJINSIA KWA WATOTO

🔘 Katika kupambana na UKATILI WA KIJINSIA KWA MTOTO, wazazi wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika mapambano hayo, hivyo ni muhimu wazazi na walezi wakumbuke au wakumbushwe majukumu yao ya malezi kwa watoto.

🔘 Siku hizi wazazi na walezi wengi wameelekeza nguvu zao kwenye kutafuta pesa, kujali pesa, na kufikiri kuwa pesa ndio kila kitu, na sio kulea watoto. Bila shaka mimi, wewe, yule, na wadau wengine tuendelee kuzidisha kasi ya kutoa elimu kwa wazazi ambao wamekuwa wakatili wa kuumiza watoto wao, na waliotupilia mbali majukumu yao ya kulea watoto.

🔘 Kutokuwepo (kusuasua) kwa malezi bora kwa watoto kunasababisha madhara mengi ikiwemo;
(a) Watoto wanaacha shule,
(b) Watoto wanapata mimba,
(c) Watoto wanabakwa/wanalawitiwa,
(d) Watoto wanaambukizwa magonjwa ya zinaa.
(e) Watoto wanauawa, wanachomwa moto.

🔘 Hivyo, (mimi, wewe, na yule) tukiwa kama wazazi na walezi, tunapaswa kufanya yafuatayo ili kumlinda mtoto;

Kuacha ukatili ambao hata wanyama hawafanyi kwa watoto wao.
Kuwa karibu na watoto wetu.
Kufuatilia maendeleo ya watoto - mashuleni.
Kuhakikisha watoto wanarudi ndani mapema (nyakati za jioni).
Kutowalaza watoto na wageni kwenye chumba kimoja.
Kuwazuia watoto wasizurure maeneo ya starehe (Bar, vilabuni, n.k).
Kuwapa nafasi watoto kujieleza ili kubaini maovu na matukio wanayotendewa.

🔘 MWISHO: "Wazazi na walezi wengi hawana elimu hii hivyo wakipewa elimu, kwa pamoja jamii tutaweza kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa mtoto".
_________
RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM

20241109_073644.jpg
 
Wazazi wa sasa, sisi kama wtt wazee wetu walitutafutia lkn pia walitekeleza wajibu wao wa kutulinda.
Sisi imekuwa tunatafuta hata hatujulikani tunatafuta nini.
Mama, baba wote wakitoka asubuhi kurudi usiku.
Watt wanaachiwa afisa malezi ambae hata kufahamu backgrounds zao hatuzifahamu.
Tukitoka wtt wamelala, tukirudi wtt wamelala.
Kwa kweli wazazi inabidi tubadilike Big time. Hiko tunachokitafuta hata tunapokipata kitakuwa na raha gani km tunaowatafutia washaharibiwa au kuuliwa?
Inaskitisha sana, wtt wetu wamekosa ulinzi katika jamii. Na cha kusikitisha zaidi waharibifu,mashetani huwa hawatoki mbali ila ndio hivyo hatuna muda wa kuyaona hayo
 
Back
Top Bottom