Maoni kuhusu biashara za kuagiza bidhaa katika masoko ya Mtandaoni nje ya nchi (Abroad Online Market)

EEM M

JF-Expert Member
May 20, 2022
422
837
Habari za Muda wana jf na natumaini wote ni wazima.

Bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye mada.

Binafsi nimekuwa nikiagiza vitu online hasa aliexpress na mara moja moja kikuu. Nimetokea kutamani sana hii fursa na kuifanya kama sehemu ya plan C katika kutafuta kusukuma ndinga kama Fortuner.

Natamani kufungua ofisi itakayokuwa inajihusisha na kununulia watu na makampuni vitu online kutoka katika mitandao ya kuaminika kama aliexpress, alibaba, ebay, Zara n.k kisha kuwapelekea.

Yani, kama mtu au kampuni itahitaji kitu flan labda kutoka aliexpress, mimi nitakuwa kama mediator ananitumia picha then mm naagiza kwa niaba yake na kumkabidhi mzigo wake.

Naomba kufahamu vitu kadhaa kuhusu hii biashara kwa mwenye experience katika mambo yafuatayo:-

  • Nawezaje kuifanya ikawa na faida?
  • Nini risk ya hii biashara?
  • Changamoto zipi zinaweza kutokea?
  • Uhakika wa kuagiza mzigo mkubwa na ukafika salama

Au chochote ambacho natakiwa kukifahamu kabla ya kujitosa huko.

Nakaribisha mawazo hasa kwa wenye experience na hii biashara.

PM yangu iko wazi ila hapa patapendeza zaidi.

Thanks, Karibu tujadili pamoja!...
 
Back
Top Bottom