Yusufu R H Sabura
JF-Expert Member
- Jun 26, 2020
- 289
- 418
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nathubutu kuandika uzi huu kulingana na experience yangu na hizi shule, lakini pia kile ambacho mimi naona kingefaa.
Hapo zamani ilikuwa ni hadithi tu kwa baadhi ya matukio ya kutisha na yasiyo ya kistaarabu kutoka katika shule za bweni hususan zile za jinsia moja. Hali ilikuwa hivyo mpaka pale ambapo Waziri mstaafu wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, Dr Harrison Mwakyembe, pamoja na mwandishi wa habari za uchunguzi, mwanadada Catherine Kahabi walipokuja na ajenda yao ya kuwalipua mashoga na wafadhili wao, hapo ndipo yaliwekwa wazi mengi yanayoendelea huko kwenye mashule ya bweni.
Si lengo langu kuwajadili mashoga hapa, ispokuwa tu, nataka kushauri namna moja ya kupunguza njia mojawapo inayozalisha binadamu wa sampuli hii.
Mimi ni miongoni mwa, kimsingi waliopata bahati ya kusoma katika shule za bweni kuanzia shule ya msingi hadi high school. tena ingekuwa afadhali kusoma shule ya bweni, nimesoma seminary ya kiislamu huko mwanza, kwahio naweza kuwapa alert ndugu wasomaji kuwa, anayezungumza ni hakika mwanaseminari.
Naomba kabla ya kupewa matusi na kulaumiwa, kwanza nianze kwa kutambua umuhimu wa uanzishwaji wa shule za namna hii.
Shule zote za bweni eidha mchanganyiko au jinsia moja, huanzishwa kwa makusudio makubwa ya kupata vijana walio na umahiri mkubwa sana katika utendaji kulingana na malengo ya waasisi wa shule husika. hiyo ni kusema kwamba, wakatoliki huanzisha seminary zao kwa malengo ya kupata wasomi wa kikristo wenye uwezo mkubwa sana ili kuweza kuitumikia dini yao katika nyanja mbalimbali ikiwemo kisiasa,kiuchumi na kijamii, mutatis mutandis kwa seminary za kiislamu.
Ipo hivi, mara nyingi sana watoto wengi hupelekwa kuanza shule wakiwa katika usawa kabisa ispokuwa wachache wenye changamoto za kimaumbile(nimeona mmoja tu miaka yote hiyo). Changamoto inayojitikeza hapa ni ileeee, tunarudi kwenye tabia za binadamu.
Kuna binadam sijui huwa wanazaliwa vp! kwa sababu binadam anaanza kuonesha tabia halisi tangu akiwa mdogo, ndio kusema, katika lilelile kundi la watoto huwa anatokea mjinga mmoja tu atakaewashawishi wenzake kujaribu tabia za hovyo(yeyote). iwapo mtoto huyo anakuwa na ushawishi kuliko mwenzake hapo ndo safari huwa inaanzia hapo tena usiri ndio huwa unatawala.
Lakini wakati mwingine huwa ni walimu walezi kabisa ambao wanashiriki katika jinai hii ya kuharibu watoto wa watu. Unakuta jamaa anakuwa anakaonesha upendo katoto ! unajua boarding hakuna wa kukujali, kwahio kwa vile mtoto anahitaji hisia zake zizingatiwe wakati wa njaa, adhabu au taabu zingine, kweli anaona ebooo ! nimepata baba. Baadae Mwalimu hutafuta mazingira ya faragha na kumharibu mtoto, then mtoto ataambiwa awe msiri vinginevyo bakora zitahusika na hatimae mtoto anamaliza shule akiwa ni bingwa wa homosexulity kwa vile atakua anazoea hivyo.
Wapo ambao huwa mungu anawabariki na kuacha kabisa mapema, lakini wapo wenye bahati mbaya huwa wanakuwa wakiwa katika hali hiyohiyo na baadae ndo kuitwa mashoga na wasagaji. asilimia kubwa ni watu ambao hawakuzaliwa hivyo bali wametengenezwa eidha kwa bahati mbaya au kwa makusudio ya waliowatengeneza.
Hivi karibuni sote ni mashahidi yapo mavuguvugu yanayotoa muelekeo wa moja kwa moja ya kutetea, na mengine yanatumia njia ya mzunguko kutetea mapenzi ya jinsia moja kwa kudai kuwa ni haki ya msingi ya binadamu. hayakuanza leo, ispokuwa tu yamechelewa kutufikia tu.
Kama nilivyozungumza mwanzo sina lengo la kuwasimanga, ispokuwa kushauri namna ya kuepusha watoto wetu kupatwa na hali hii ya kuwataka kingono wanaume au wanawake wenzao.
Kama taifa tunapaswa kupitisha azimio la kupiga marufuku shule hizi za jinsia moja.
Najua hapa nitaonekana kuingilia imani za dini nyingine lakini kwa vile zipo hata za dini yangu nitajikita huko. nitashauri au kupinga moja kwa moja shule za kiislamu za jinsia moja kwa vile hawa ninawaweza. waswahili wanasema mtoto akikunyea mkono hauukati. Uislamu ndio mzazi na mlezi wangu.
Ninatambua kabisa marufuku iliyopo katika dini yetu ya kupinga faragha kati ya jinsia mbili tofauti, hili haliruhusiwi na sipo hapa kupigia chapuo faragha ya mtu.
Serikali na ndugu waislamu, sasa nazungumza na nyinyi kwa sababu nawaweza ;
Ili tuikomboe jamii ya kitanzania kutoka kwenye minyororo ya mavuguvugu haya ambayo yanakinzana kwa asilimia zote na mila na tamaduni zetu, hatua ya kwanza kabisa ambayo nafikiri ingefaa ni kuzuia kabisa kama sio kupunguza machimbuko ya michezo hii. sijui ni nani atabisha kuwa mashule sio machimbuko ya hii michezo mbele ya ushahidi uliowekwa na mzee Mwakyembe na mwenzake Catherine.
Tuzuie shule za kiislamu za jinsia moja na tuwachanganye ili mtoto akue akijua kwamba binadamu tumeumbwa kwa pair, na pair yenyewe ni jinsia nyingine(aione ipo hapo) ambayo ipo siku atakabidhiwa iwapo atatimiza vigezo vya kisheria.
Hata kama watoto hawaruhusiwi kupendana lakini ni lazima katika makuzi yake tayari atakuwa na jina la binti ambaye akimuona tu moyo utashtuka ! (hili sio kosa kidini wala kiserikali). hii itasaidia kupunguza au kuondoa kabisa hisia au tabia hasi inayoweza kumsogelea.
Utaratibu wa kiislamu wa kuwatenganisha wanaume na wanawake utaendelea vilevile kwa, kuwatenganisha kimistari tu wawapo madarasani, lakini mavazi na tabia za kiislamu zibaki palepale, lakini pia lisiwepo pazia la kuzuia kuonana wala kuzungumza. waacheni watoto wazungumze lakini wanyimeni faragha tu.
Serikali na ndugu waislamu, kufanya hivi ni bora zaidi kwa vile ;
* tutakuwa hatujafanya kosa kidini, hatutaenda peponi kwa sababu tulijenga seminary bali tutaenda peponi kwa matendo yetu mema.
* Lakini pia hata yanayofundishwa seminarini(islamic) siyo utengano kati ya mwanaume na mwanamke bali matendo mema hivyo useminary ni jitihada tu.
*Angalau tutakuwa tumekiepusha kizazi cha watanzania na tabia mbaya.
Ninafahamu kuwa ubishi kwa waislamu ni suala la kihistoria na huwa tunashtuka muda ukiwa umekwisha lakini hili sidhani kama mtalibishia kwa vile hata mtume wetu sidhani kama anaijua seminari.
Asante na Kazi Iendelee
0750883466/0717934194.