Maombi ya kujengewa uwanja wa Basketball Toangoma wilaya ya Temeke

Mar 9, 2023
36
52
Ndugu zangu nimekuwa nikiwaza ni jinsi gani ntaweza kusaidia kujenga uwanja wa BASKETBALL mtaani kwangu kwa muda mrefu sasa, sina kiasi cha pesa cha kutosheleza kwasababu mimi pia ni mwanaharakati wa hapa na pale ili nipate kula.

Katika kukaa na kutafakari nkagundua kwamba naweza nikakutana na watu hawa na wakaweza kutusaidia kujenga uwanja wa BASKETBALL ndani ya TOANGOMA-TEMEKE, watu hao ni

1. MKUU WA WILAYA YA TEMEKE

2.MBUNGE WA ENEO HILI

lakini tatzo kwangu linakuwa moja tu, je ntawafikiaje watu hawa wenye nyazifa serikalini, je niwatembelee maofisini kwao au niandike barua na je kama nikiwatembelea ntapata nafasi ya kuwaona au ndo mpaka na mi niwe na connection ili kukutana nao.

Kiukwel vijana wa toangoma tulijitahidi kwa kiwango chetu kujenga robo uwanja na tukaweka goli moja ambalo ni muda sasa sisi kama vijana jion hukutana kufanya mazoezi ya pamoja na inatusaidia kutuleta pamoja na kudumisha undugu baina yetu.

Lakini hadhi ya kiwanja haifai hata kidogo, imefikia sehem sasa kunakuwa na vishimo katika uwanja, hali inayopelekea maumivu ya ankle mara kwa mara kwa wachezaji.

NAOMBENI USHAURI WENU KWA WENYE UZOEFU NA WALE AMBAO MNA NAFASI ZA JUU SERIKALINI MNAKARIBISHWA KWA MSAADA.

Je ni kwajinsi gani ntawafikia viongozi hawa wa wilaya ili niwaeleze changamoto yetu ya uwanja, kwa yeyote mwenye ushauri naupokea.
 
Hao hawawezi kukusaidia ongea na wadau wa mashirika au kampuni au watu binafsi
Ila mwanasiasa achana nae kabisa
Hapa umemaliza kila kitu.
Huu ndio mpango kamili.

Kutaka kumsaidia mleta mada, afanye haya.
1. Aandike mpango wake kamili chini akihusisha makadirio ya gharama, umiliki wa kisheria utakuwa kwa nani, faida za kijamii na faida watakazopata wadhamini.
2. Aanishe na kuthibitisha uwepo wa eneo
3. Atafute uungwaji wa mkono kutoka chama cha mpira wa kikapu kutoka wilaya nk.
4. Ajiongeze kwa kuanzisha harakati za watu kucheza huo mchezo kwenye hilo eneo.
 
Umeweka kitaalam zaidi labda hapo kwenye kuandika ndio atafute msomi mmoja amsaidie waandike Kisha atakeleze
 
Hapa umemaliza kila kitu.
Huu ndio mpango kamili.

Kutaka kumsaidia mleta mada, afanye haya.
1. Aandike mpango wake kamili chini akihusisha makadirio ya gharama, umiliki wa kisheria utakuwa kwa nani, faida za kijamii na faida watakazopata wadhamini.
2. Aanishe na kuthibitisha uwepo wa eneo
3. Atafute uungwaji wa mkono kutoka chama cha mpira wa kikapu kutoka wilaya nk.
4. Ajiongeze kwa kuanzisha harakati za watu kucheza huo mchezo kwenye hilo eneo.
Tayar vijana wapo na wanacheza kila siku, na ni mwaka sasa tunatumia kiwanja hicho kama mazoezi
 
Hapa umemaliza kila kitu.
Huu ndio mpango kamili.

Kutaka kumsaidia mleta mada, afanye haya.
1. Aandike mpango wake kamili chini akihusisha makadirio ya gharama, umiliki wa kisheria utakuwa kwa nani, faida za kijamii na faida watakazopata wadhamini.
2. Aanishe na kuthibitisha uwepo wa eneo
3. Atafute uungwaji wa mkono kutoka chama cha mpira wa kikapu kutoka wilaya nk.
4. Ajiongeze kwa kuanzisha harakati za watu kucheza huo mchezo kwenye hilo eneo.
Kuhusu umiliki wa kisheria naomba niongeze jambo, huu uwanja upo sehemu ambayo ni eneo maalumu lililotengwa na serikali kwaajili ya michezo, kama tunavyojua serikali hutenga maeneo ila kuhusu ujengaji wa viwanja ni juu ya wananchi.

Ndoo maana nkaanza kusema je kunauwezekano kuifikia serikali ili ikamilishe yenyewe kuepusha mambo ya umiliki
 
Hao hawawezi kukusaidia ongea na wadau wa mashirika au kampuni au watu binafsi
Ila mwanasiasa achana nae kabisa
Hakuna namna tunaweza msulutisha mwanasiasa na akafanya kazi yake kwa usahihi, maana hii swala la kujengewa viwanja liko chini ya serikali iliyotenga maeneo kwaajili ya viwanja
 
Back
Top Bottom