Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,209
- 2,953
Mtu Mmoja aliyefahamika Kwa jina la Yona Andrea (47) Mkazi wa kijiji cha loltepesi kata ya Sunya wilayani kiteto Mkoani Manyara, ameuwawa Kwa kupigwa na kitu kizito na watu wasiojulikana huku mkewe Catherine Andrea (45) akijeruhiwa mara baada ya kuvamiwa katika nyumba yao.
Tukio hilo limetokea Oktoba 12, 2024 mara baada ya Watu hao wasiofahamika kuvamiwa nyumbani Kwa marehe na kumtaka mke wa marehemu kuwapatia kiasi Cha Tsh. laki nne (400,000/=) fedha ambazo ni za kikundi Cha Kicoba alizokuwa amehifadhi.
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Remidius Mwema amekemea vitendo vya ukatili vinavyofanywa na wananchi na kuwaasa kuacha vitendo hivyo vya ukatili na kujichukulia sheria mkononi, pia amewataka kushirikiana katika kudumisha amani na utulivu katika jamii.
Video: Global TV