Manka mbaroni kwa kumchoma moto msaidizi wake wa ndani kwa mafuta

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,067
10,936
Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linamshikilia Christina Shiriri (43) kwa jina maarufu Manka, mfanyabiashara na mkazi wa Usagara wilaya ya Misungwi kwa kosa la kumfanyia ukatili mfanyakazi wake wa ndani Grace Joseph (17), mkazi wa Kijiji cha Nyalwigo wilaya ya Misungwi kwa kummwagia mafuta ya taa mwilini kisha kumchoma moto akimtuhumu kumwibia fedha kiasi cha Tsh. 161,000.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Wilbrod Mutafugwa Jumatano Juni 05, 2024 imeeleza kuwa tukio hilo lilitokea Juni 4, 2024 katika kata na tarafa ya Usagara wilaya ya Misungwi ambapo Christina Shiriri alidai kuibiwa fedha zake alizokuwa amehifadhi chumbani kwake na alipomuuliza binti yake wa kazi alikiri kuchukua fedha hizo na kuamua kumrejeshea.

“Baada ya kurejeshewa fedha hizo Christina Shiriri aliamua kumfanyia ukatili binti huyo kwa kumchoma moto mikono yote miwili, tumboni pamoja na mapaja yake yote mawili.Grace Joseph amepelekwa katika hospitali ya wilaya ya Misungwi kwa ajili ya matibabu. Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa kwa kina na atafikishwa mahakami mara baada ya upelelezi kukamilika” Amesema Kamanda Mutafungwa.

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limetoa rai kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi wakati wanapowatuhumu watu wanaofanya makosa, badala yake wawafikishe kwenye vyombo vya sheria kwa ajili ya hatua za kisheria.

Chanzo: Jambo tv
 
Manka mwenyewe sasa
1717597318481.jpg
 
Mwizi pekee anayestahili huruma ni yule anayeiba chakula au kitu chochote kwasababu ya njaa.
The rest must experience hell on Earth.
Nice move Manka.
 
Makatili hao wanawatesa wanafanyakazi wa ndani sana , maana ukitaja hapa utaambiwa unawachukia.
 
Sasa uchunguzi ukamilike vipi wakati mtuhumiwa kamchoma Moto mtu na inajulika sasa wanataka kikamilike nini?
 
Wamchome uchi wake aone utamu wa moto.

Angemfukuza huyo binti badala ya kumchoma.
 
Back
Top Bottom