Bado Hujasema
Member
- Dec 1, 2024
- 10
- 12
Mimi ni Mfanyabiashara wa Soko Kuu la Chifu Kingalu ambalo lipo Manispaa ya Morogoro, katika soko hili kuna changamoto kubwa hasa kuharibika kwa taa, swichi za feni pamoja na masinki ya kunawia mikono.
Tangu soko lifunguliwe Mwaka 2020 halijawahi kufanyaiwa ukarabati, hivyo taa haziwaki mpaka tunahofia mali zetu kuibiwa hasa nyakati za usiku.
Kwa upande wa masinki ni mabovu mpaka yanasababisha maji hayapiti vizuri, hii ni mbaya sana ukiangalia soko hili ni kubwa na watumiaji ni wengi, pasipokarabatiwa hali itazidi kuwa mbaya sana.
Tumejaribu kuulizia kuwa ni gharama kiasi gani zinaweza kutumika katika kukarabati vitu vyote hivyo, ambapo tumeambiwa ni shilingi laki 8 tu za kitanzania zinaweza kuweka mazingira sawa hapa.
Lakini tunashangaa kwanini hapakarabatiwi na kibaya zaidi tumeomba kufanyiwe ukarabati.
Hapa sokoni kwa mwezi zinakusanywa Shilingi milioni 74 kwa ajili ya mapato, hivi kweli laki 8 inashindikana kutolewa ili pawe salama humu ndani?
Tunauomba Uongozi wa Manispaa ya Morogoro kuangalia hili suala maana tushaomba sana ukarabati ufanyike lakini mpaka sasa hakuna utekelezaji, hii ni mbaya sana.
Soko limeshafikisha miaka minne mpaka sasa lakini hamna maboresho hayo mapato yanayoingizwa ni ya nini mwisho wa siku lije nipoteze mvuto watu wahame humu mapato yakosekane tuwe na utaratibu wa kuvipenda vitu vinavyotuingizia fedha.