KERO Manispaa ya Kinondoni inatoza gharama kubwa kwenye sticker za matangazo zinazobandikwa kwenye milango

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kuanzia mwezi Julai mwanzoni mpaka sasa manispaa inayohusika na maeneo ya Makumbusho wanatoza gharama kubwa kwa ajili ya matangazo wanayobandika wafanyabiashra kwenye milango yao ya maduka bila ya kuzingatia aina ya biashara anayoifanya mtu.

Unakuta mtu ana mtaji mdogo ameweka matangazo hata ya kutengeza kucha wanatoza mpaka laki nane kitu ambacho kinawashangaza wengi.

Mtu unakuta unatozwa gharama kubwa kuliko hata unayolipia TRA kitu ambacho kinatukwaza wafanyabiashara wa maeneo ya Makumbusho na hatuna sehemu ya kwenda kulalamika.
 
Pole sana
Watumieni madawani wenu, hili lipo ndani ya uweZo wao
 
Kwamba mtu unalipia tangazo uliloweka kwenye mlango wa duka lako?

Kisha hayo malipo yanakwenda kwa nani manispaa au waliowapangisha maduka?
 
Kuanzia mwezi Julai mwanzoni mpaka sasa manispaa inayohusika na maeneo ya Makumbusho wanatoza gharama kubwa kwa ajili ya matangazo wanayobandika wafanyabiashra kwenye milango yao ya maduka bila ya kuzingatia aina ya biashara anayoifanya mtu.

Unakuta mtu ana mtaji mdogo ameweka matangazo hata ya kutengeza kucha wanatoza mpaka laki nane kitu ambacho kinawashangaza wengi.

Mtu unakuta unatozwa gharama kubwa kuliko hata unayolipia TRA kitu ambacho kinatukwaza wafanyabiashara wa maeneo ya Makumbusho na hatuna sehemu ya kwenda kulalamika.
hao jamaa wanatoza gharama kulingana na ukubwa wa tangazo lako (upana na urefu) hilo tangazo lako lina ukubwa gani?
 
Back
Top Bottom