Mangwair vs Chid Benz

central midfielder

Senior Member
Apr 14, 2023
146
215
Ndugu zangu wa Hip hop nawaomba hapa kidogo tuwekana sawa.

Wanasema kwenye pick yake The Late Albert Mangwair alikuwa mkali sana wa freestyle yani mitindo huru. Na sifa kuu alikuwa na uwezo mkubwa wa kukaa kwenye topic bila kutoka nje ya mada huku akifreestyle tu(nlimsikia juzi kati fareed kubanda akisema hili)

Lakini wanasema Rashid Makwilo yani Chid Benz pia alikuwa noma sana kwenye mitindo huru.

Kwanini nimeandika haya????

Wanasema kuna battle ilifanyika kati ya Chid na Mangwair na Chid Benz alipotezwa vibaya mno tena alikuwa nyumbani Ilala.

Ebu kwa anaefahamu je ni kweli??? Na ulikuwa mwaka gani?

Ngwair na Chid nani zaidi????

Karibuni.
 
Hao wote ni overated. Labda kama mnazungumzia freestyle (kwa maana ya kuflow bila kuandika), ila kwenye uandishi Kuna watu wanasubiri sana
 
Alivokua mangwair zamani ni mara mbili ya marapa wote wa sasa hivi
 
Uyo Ngwea alikua mbele ya wakati.. Chid kawaida sema sauti na vibe.
 
Mara ya kwanza mi namuona, East Zoo' Dodoma🎶
Ghafla nikajihisi kama mtu mwenye homa 🎶
Kutoa salamu tu jibu lake ni noma🎶
Sauti yake tu nikajihisi nimepona🎶
Ndefu yake shingo, mwendo wa maringo Oh oh
Nilifurahi aliponiambia yuko single🎶
Sio siri mtoto huyu ameumbika🎶
Na kama akipita' mbele ya watu kumi basi Nane kati yao lazima watababaika🎶
Hata hao wawili wivu tu umewashika
Yessir'
Mangwair ndio amefika' 🎶
 
Ndugu zangu wa Hip hop nawaomba hapa kidogo tuwekana sawa.

Wanasema kwenye pick yake The Late Albert Mangwair alikuwa mkali sana wa freestyle yani mitindo huru. Na sifa kuu alikuwa na uwezo mkubwa wa kukaa kwenye topic bila kutoka nje ya mada huku akifreestyle tu(nlimsikia juzi kati fareed kubanda akisema hili)

Lakini wanasema Rashid Makwilo yani Chid Benz pia alikuwa noma sana kwenye mitindo huru.

Kwanini nimeandika haya????

Wanasema kuna battle ilifanyika kati ya Chid na Mangwair na Chid Benz alipotezwa vibaya mno tena alikuwa nyumbani Ilala.

Ebu kwa anaefahamu je ni kweli??? Na ulikuwa mwaka gani?

Ngwair na Chid nani zaidi????

Karibuni.
Wote hao wapo overated .
 
Kwa Uwezo aliokua nao Mangwea ,ni matusi kumlinganisha na Chidibenz

Chidibenz hajui freestyle kabisa coz akifanya frestyle anaongea vitu ambavyo havina maana yoyote ,ukitaka kuamini ,mtafute chidibenz kwenye Dakika kumi za maangamizi pale East africa radio

Sent from my SM-A235F using JamiiForums mobile app
 
Kwa freestyle ngwair ni balaa, chid huwa anavuruga vuruga tu ila ana sauti flani na vibe.

Kuna kipindi cha dk 10 za maangamizi alikuwa marehemu zillah, aiseh lile jamaa ni balaa kwenye freestyle, ananata na biti, hatoki nje ya kike anachokiimbia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom