Mangula na Kinana wanaweza kuendana na kasi ya Rais Magufuli ndani ya CCM na si Rajab Luhwavi

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,374
Wadau, amani iwe kwenu.

Nimewaza na kutafakari sana. Nikafikiria na Kushirikisha ubongo wangu. Hakika naiona CCM yenye nuru na mwanga angavu. Naam CCM inazaliwa upya Julai 23 pale tutakaposhuhudia Comredi John Pombe Magufuli akichaguliwa kwa kishindo kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM, nafasi atakayohudumu hadi 2017 tutakapofanya uchaguzi kwa ngazi zote za chama kuanzia Mwenyekiti taifa hadi huko kwenye matawi.

Leo tunapochagua Mwenyekiti ni 2016 na Uchaguzi Mkuu wa chama utafanyika 2017. Kwa maana hiyo mpasa sasa Julai, ni muda wa chini ya mwaka mmoja umebaki ili tuingie kwenye uchaguzi.

Tunapoelekea 2017, baadhi ya makada wameshajiposition kwenye nafasi wanazotaka. Ni kama vile walivyokuwa wanafanya baadhi ya Maafisa pale Utumishi kwenye nafasi za Uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri. Ndivyo ilivyo kwa CCM sasa. Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajab Luhwavi anahusika na mchezo huu mchafu. Kwa kipindi kifupi alichokaa madarakani ambacho ni mwaka mmoja tu, tayari ameshahamishia Makao Makuu ya CCM baadhi ya watu ambao anadhani kuwa watamsaidia katika kutekeleza mikakati yake anayofikiria. Sina sababu ya kuwataja ila wenyewe wanajijua. Zile ndoto za Comredi Kinana za kuwa na CCM imara inayoweza kuisimamia Serikali ipasavyo inaelekea kuyeyuka.

Mwenyekiti Mtarajiwa alitoa Ombi kwa Mwenyekiti kuwashughulikia wale wote waliokihujumu chama wakati wa Uchaguzi Mkuu. Hata hivyo, mpaka sasa, sijaona mtu yeyote akiwajibishwa kutekeleza ombi la Mwenyekiti mtarajiwa. Siwezi kumlaumu Kikwete kwa vile si kila mtu ana uwezo wa kufanya maamuzi. Uwezo huo anao Magufuli, Mangula na Kinana. Haya ndio majembe ya CCM ambayo hayana simile katika kuwajibisha.

Kukabidhiwa kwa Magufuli chama maana yake ni kwamba kuna watu wapo matumbo joto mpaka sasa. Wanajua kuwa Magufuli atasafisha chama kuanzia pale Makao Makuu kama alivyofanya Ikulu. Wale wote wanafiki, wasaliti na wahujumu hawatabaki salama. Naamini kuwa Uwezo wa kusafisha chama anao Magufuli. Hata hivyo, anahitaji usaidizi wa watu sahihi. Kwa mtazamo wangu, Mangula na kinana wanaweza kumsaidia Magufuli kusafisha chama kwa vile walishathubutu kufanya hivyo na dhamira yao inaonekana.

Dua na sala yangu siku zote ni kuona hawa ma Comredi watatu wakichapa kazi pamoja hata kama ni kwa kipindi cha mwaka mmoja ili wakinyooshe chama. Naam ni Magufuli, Mangula na Kinana ama kwa kifupi MMK. MMK ni dawa ya maovu yote yaliyopo ndani ya chama. Sina shaka na dhamira njema ya MMK katika kudhibiti maovu yote ndani ya chama. Sina shaka na Uwezo wa MMK katika kukabiliana na wale wote wanaojiona ni miungu watu ndani ya CCM. Nina hakika kuwa MMK hawatajali sura ya mtu wala uwezo wake kifedha katika kuadabisha. CCM imara huzaa Serikali Imara. CCM legelege huzaa Serikali legelege.

Kwa Muktadha huo, kwa vile muda uliobaki hadi tufanye tena Uchaguzi Mkuu ndani ya chama ni mfupi, na kwa kuwa Mwenyekiti mtarajiwa anahitaji kupata usaidizi wa karibu kutoka kwa mtu sahihi mwenye mawazo sahihi na mtazamo chanya kwa chama, ni mtazamo wangu kuwa Magufuli awe Mwenyekiti na kama itampendeza, Makamu Mwenyekiti abaki Mzee Philip Mangula na Katibu Mkuu aendelee kuwa Comredi Kinana. Naibu Katibu Mkuu Bara ajiondoe mwenyewe kabla hajafukuzwa. Uongozi wa CCM kwa upande wa Zanzibar ubaki kama ulivyo hadi 2017 tutakavyofanya uchaguzi.

Kwa kifupi ni kwamba kwa vile Kikwete ameridhia kuondoka, aondoke na Rajab Luhwavi ambaye ni dhahiri kwamba hayupo katika muelekeo wa CCM mpya tunayoitarajia. Huu ni mtazamo wangu na unaweza usishabihiane na mtazamo wa wadau wengi hapa JF.
 
Ni kweli ni mtazamo wako.......

Ila realty Kinana ni mtu mwenye kufikiri kabla ya kutenda sasa sijui huyu bwana atafanya vp kazi na hiyo timu uliyompangia (MMK).

Any way, ..........
Adui mwombee njaa. Nakutakia ndoto njema
 
Ningependa kinana apumzike kazi aliyofanya ni kubwa sana!!
Upo sahihi kabisa. Ila kwa vile tupo kwenye transition, napendelea Kinana aendelee kubaki hadi 2017 kwa vile naamini kwa sasa itafanyika reform kubwa kwa watendaji wa chama ambapo Kinana anapaswa kushiriki kwa vile anawafahamu vizuri watendaji wake.
 
Mie nakereka kweli na hizi post za kuhusu chama changu na haya makabidhiano ya uenyekiti, hivi nyie wanaCCM wenzangu mna sababu zipi za kuanika masuala ya chama hapa JF? halafu mbaya zaidi mnaanza hata kutoleana lugha ambazo sio nzuri! Hebu tulieni acheni makundi makundi, kama nyie ni wajumbe wa mkutano mkuu sawa endeleeni na maandalizi ya kwenda Dodoma kama sio wajumbe kama mimi naomba mtulize ndimi zenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…