Mangi aingizwa cha jiji

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
283,653
737,227
Kama ulikua hujui kuwa duniani kuna MCHAGA amewahi kutapeliwa MILIONI SITA NA KUPEWA SANDUKU wacha nikufahamishe;-
Katika hali isio kuwa ya kawaida kuwahi kutokea duniani,
Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la POLINARY MWANGA,
Ambae ni mkazi wa KIBOSHO mkoani KILIMANJARO,
Ametapeliwa kiasi cha milioni sita na laki saba,
Na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mganga wa kienyeji,
Baada ya kwenda kwa mganga huyo akitaka utajiri,
Ili kuondokana na umaskini katika maisha yake,
Akiongea na chombo kimoja cha habari POLINARY alisema kuwa;-

"Nilipata milioni sita na laki saba nikaamua kwenda nazo kwa mganga ili nipate utajili,
Nilipofika mganga aliniambia hilo ni jambo rahisi sana,
Kwani hiyo ndio shughuli yake inayo muweka mjini,
Na watu wengi wamepata utajili kupitia yeye baada ya kutoa kiasi kidogo cha pesa walicho nacho,
Alinitajia majina ya watu wengi matajili akisema kuwa,
Watu hao wote wamekua matajili kupitia yeye,
Aliposema hivyo nilishawishika na kumuamini,
Akaniuliza unataka uwe tajili kama nani hapa Tanzania,
Nikamwambia nataka kuwa tajili kama MENGI,
Mganga akaniambia hilo limeisha lakini,
Natakiwa kutoa pesa yote niliokuwa nayo,
Na akasema kadri ninavyotoa pesa nyingi ndivyo nitakavyo kuwa tajili zaidi kuliko mtu nilie mtaja,
Basi nikamwambia mimi nina milioni sita na laki saba,
Mganga akasema tena hiyo ni nyingi sana,
Hiyo pesa nikitoa nitakua tajili kuliko mengi na nitamfikia BAKHRESA,
Nikafurahi kusikia hivyo kwasababu nauchukia sana umasikini,
Na hiyo pesa niliokuwa nayo niliuza sehemu ya shamba langu,
Kwahiyo nilitaka izalishe zaidi na zaidi kwasababu ndio tegemeo langu,
Akaniambia toa hizo pesa zote weka kwenye hiki chungu nikaweka,
Baada ya pale mganga akaniambia subili nakuja akaingia chumbani kwake,
Baada ya muda kidogo mganga akatoka na sanduku la bati,
Ambalo mala nyingi wanafunzi hulitumia shuleni,
Akaniambia hili sanduku unaloliona humu ndani limejaa pesa tupu,
Lakini natakiwa niende kulifungulia nyumbani,
Na nikiwa njiani sitakiwi niongee na mtu yeyote,
Na nikifika nyumbani kabla sijaongea na mtu yeyote pale nyumbani na kabla sijalifungua,
Nimpigie simu kuna kitu atanielekeza kufanya,
Baada ya kufanya hicho kitu ndio nifungue hilo sanduku,
Nilivyofika nyumbani nilimpigia simu yule mganga,
Akaniambia chukua udi washa halafu simama nao hadi uishe,
Nikafanya kama alivyo nielekeza nikasimama nao hadi ukaisha,
Ulipo isha nikampigia simu tena lakini simu haikupatikana,
Nikakumbuka alisema udi ukiisha nifungue sanduku langu la pesa,
Nikiwa na furaha zote za utajili nikaamua kulifungua,
Nilipolifungua sikuamini nilicho kikuta ndani,
Kwani nilikuta magazeti kibao pamoja na biskuti,
Baada ya kuona hivyo nikampigia tena simu hakupatikana,
Nikaamua kwenda nyumbani kwake lakini sikumkuta na nyumba ilikua imefungwa,
Ndipo nilipogundua kuwa nimetapeliwa,
Na Slsasa sielewi hili sanduku na haya magazeti pamoja na biskuti nifanyie nini".....amesema POLINARY

Huyu jamaa ndio mchaga wa kwanza duniani,
Kutapeliwa pesa na mganga wa kienyeji🤣🤣🤣🤣🤣🤣.

Makala hii imeletwa kwenu na Dhulkad Madara kutoka Morogoro

Zaidi soma

FB_IMG_1733423651645.jpg
 
Wale wote wenye lafudhi za kienyeji za makabila yao ya asili hata wanapoongea lugha yetu adhimu ya kiswahili wakiwemo wachaga!, kupigwa ni rahisi sana! Hiyo ni indicator utakayoishi nayo kwa muda mrefu sana kuwa wewe ni wakuja tu.😀
 
Ndugu yangu baada ya kuuza mji wa familia wakaenda kwa mhuni,wakaambiwa waweke fedha zooote ndani chungu.
Wakapewa gunia ambamo ndani yake waliambiwa ni fedha na baadae zitajaa hilo gunia.

Waliambiwa wasioge kwa muda wa siku 60 bali wawe wanapakaa mafuta waliyopewa na huyo mhuni,sasa kadri siku zinavyo songa mbele,ndivyo gunia linavyo tuna.

Watu wakaendeleza mgomo wa kutooga na tambo nyingi kitaani huku utajiri ukikaribia.
Siku ya 60 watu kimuemue kiko kileleni.

Siku 61 kufungua laaulaaa majani ya mahindi yamekauka vizuuuri na kulitunisha gunia,ongezea na kelele zake sasa zilivyokuwa zikiongezeka kila yalipokuwa yakizidi kukauka.

Kilichofuatia huyo mama yangu makazi yake ilibidi tuyahamishie hospital,mabinti zake sasa ukijumlisha kutokuoga huo muda waliokuwa wamepewa majani ya mahindi tangu yakiwa mabichi mpaka kukauka wanatoa harufu siyo ya nchi hii halafu pesa zikayeyekaa!

Mpaka ninaandika hapa mama mdogo ni mzima
Lkn hana makazi,amepanga.
 
😭😭😭
 
Si semi kwamba sijawahi kutapeliwa lakini sio kiivyo kama huyo mchaga😆.
Kuna mwana JF mwenzetu alitapeliwa milion 32 tasilimu maana 2020 nadhani kule Morogoro aliuza hadi nyumba yake nakumbuka.
Kama yupo hapa na anausoma huu uzi kwa ruhusa yake nitasimulia A to Z kilichompata.. Naye ni huu huu utajiri wa begi
 
Huyu mchaga toleo la mwisho. Hakuna mchaga mjinga kiasi hiki

Hata ukoo wake haujakaa kichaga
Mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la POLINARY MWANGA,
Ambae ni mkazi wa KIBOSHO mkoani KILIMANJARO,
 
Back
Top Bottom