GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,280
- 6,684
Nakumbuka miaka mingi nyuma nikiwa mdogo, Naenda hospitali kuchoma
sindano. Nesi anakuchoma sindano huku anakubembeleza "Pole... eeh, pole
Baba'angu... utapona tu"
Manesi walikuwa wapole wenye maneno ya kuliwaza, waliwajali na kuwapenda
wagonjwa wakiwa na MAVAZI YAO MEUPE yenye kuvutia. Wengi wao walikuwa
ni manesi wenye elimu ya Darasa la saba tu lakini ajabu walikuwa vizuri utafikiri
wamepitia vyuo vya udaktari.
Walihudumia wagonjwa na kuhakikisha mazingira yanakuwa safi, kama ulikuwa
hujazaliwa kipindi hicho basi nikueleze tu kuwa kipindi hicho hospitali za serikali
hazikuwa chafu kama unavyoziona leo.
Wale Manesi ambao walikuwa wanavaa mavazi meupe wakanyang'anywa mavazi
yao wakapewa hawa wa kizazi kipya, FORM FOUR ikawabeba, hapo ndipo nilipoanza
kushuhudia tabia za manesi hawa WASOMI, hawana heshima wala nidhamu
wengi wao ni wakali na wakatili. Mavazi meupe wanayovaa hayaendani na tabia zao
waulize kina mama wanaoenda kujifungua kwanza........ ni mabingwa wa matusi
Lakini nimalizie kwa kusema sio wote, wapo wastaarabu wanaotambua misingi ya kazi
zao.
Yote kwa yote lazima wakubali kuwa walimu wao halisi ni hawa wanaowakuta
maofisini hivyo musiwadharau.