Maneno yaliyosahauliwa kabisa

Kipala

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
3,763
700
Baada ya kumaliza makala kuhusu vipimo vya kihistoria vya Waswahili kwenye wikipedia nimeongea leo hii na vijana nikiwauliza kama wameshawahi kusikia maneno kama "Wanda", "Morta" au "Shibiri". Hapana. Hawakusikia. Basi nitakapofika Dar nitafanya jaribio, sokoni nitajaribu kununua machungwa, ratili moja hivi. Tuone!
Vipimo asilia vya Kiswahili - Wikipedia, kamusi elezo huru
 
Vipimo vya kizamani namna hiyo nani atavitumia leo karne hii?Kuna vitu lazima vife tu kwa sababu haviendani na spidi ya teknolojia.
Leo hii ukienda duka la muziki na kuulizia kanda ya muziki utachekwa sana, utaulizwa: wataka kanda au cd?
Hapa hakuna wa kumlaumu wala nini, ila ni vizuri tu kufahamu ya zamani just for curiosity sake!
 
Asante kwa jibu, ila tu sijamlaumu mtu yeyote.
Kuhusu "spidi ya teknolojia" - ukitaka spidi basi heri ujifunze MORTA!! Maanake mimi mwenyewe nilijifunza wakati nilipokuwa kwa maskauti ya kwamba MORTA yangu (kwa Kizungu "span ") ni takriban sentimita 20. Kwa hiyo nikitakiwa kutaja haraka upana au urefu wa kitu natumia MKONO (faida inapatikana kila wakati, sihitaji kuwasha wala haikwami au kuishia beteri !) nafungua vidole na kupima kwa MORTA. Baadaye najua urefu ni takriban sentimita 20, 40, 60, 80 hivi. Kama ni ndefu kidogo zaidi naongeza vidole kwa kuona idadi ya WANDA (kwangu sentimita 2 hivi) napata kipimo.
Hapo naona faida.

Nikihitaji kipimo kamili natafuta rula au futi; au naanza kutafuta kwenye intaneti kwa app inayopima kupitia mobile yangu....
Lakini kwa spidi: kompyuta haiwezi kushindana na MORTA - eti wazee hawakuwa wajinga tu.
 
Lakini nakiri: shibiri sina kazi nayo kweli - kwangu karibu sentimita 24, haiingii kirahisi katika makadirio. MORTA lakini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…