Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,646
Kwa mujibu wa Kanuni za Usalama wa Taifa, Uhuru wa Kujieleza na Upatikanaji wa taarifa za Johannesburg 1996; zuio kwa misingi ya 'Usalama wa Taifa' haliwezi kukubalika endapo lengo halisi ni kulinda maslahi yasiyohusiana na Usalama wa taarifa.
Zuio kwa misingi ya kulinda Usalama wa Taifa halitakubalika ikiwa ni kwaajili ya:
Kanuni za Usalama wa Taifa, Uhuru wa Kujieleza na Upatikanaji wa taarifa za Johannesburg 1996
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi 2022, ambayo imeanza kufanya kazi toka Mei 1, 2023 imetumia maneno ‘Usalama wa Taifa’ bila ya kutoa tafsiri ya maneno hayo licha ya Tanzania kuwa moja ya nchi iliyokubaliana na kanuni za Johannesburg.
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, 2022
Wadau mbalimbali wameshauri maneno 'Usalama wa Taifa' kutolewa tafsiri kwa mujibu wa sheria hii, kwasababu maneno hayo kuwepo bila ya tafsiri yanaweza kutumiwa vibaya na kuchangia uvunjivu wa haki na uonevu kwa jina la 'kuhatarisha usalama wa taifa' ama 'kulinda usalama wa taifa' na hivyo kuleta ugumu katika utekelezaji wa sheria hii.
Zuio kwa misingi ya kulinda Usalama wa Taifa halitakubalika ikiwa ni kwaajili ya:
- Kulinda serikali kutokana na aibu au kufichuliwa kwa vitendo vya uovu
- Kuficha taarifa kuhusu utendaji wa taasisi zake za umma
- Kuhakikisha mrengo fulani wa itikadi
- Kudhibiti migogoro