Kichuchunge
JF-Expert Member
- Dec 2, 2020
- 370
- 958
"Kuwa mwanasiasa na hasa Rais wa nchi ni kuwa mwigizaji. Mwanasiasa mzuri daima ni mwigizaji mzuri. Atajitia ukali mahala pasipo na ukali, kadhalika, atajitia upole mahala panapohitajika ukali; mradi dhamira yake ifanikiwe. Ni hilo ambalo huwafanya marais wote ulimwenguni kuweza kusimama mbele ya halaiki kubwa ya watu na kulaani kwa ukali kitu ambacho rohoni wanakiamini. Na siku chache baadaye wanaweza kukitetea kitu hichohicho, katika halaiki hiyohiyo; na bado wakaungwa mkono." Niliwahi kuyasoma maneno haya kwenye kitabu cha Malaika wa Shetani cha marehemu Ben R Mtobwa. Nimeyasoma kwa makini na kuyarudia tena na tena nikaona yana ukweli mwingi sana. Je, wewe unayaonaje?