Kuna walakini umejikoteza kwa klabu ya Manchester United kumnunua mchezaji Antonio Griezman wa Atlético Madrid baada ya mahakama ya kimataifa ya maamuzi ya kisoka (The Court of Arbitration for Sport-CAS), kuizuia klabu hiyo kufanya usajili mpaka mwezi wa kwanza mwakani.
Maamuzi hayo yamekuja kutokana na klabu hiyo ya Hispania kukiuka taratibu kwa kusajili vijana wadogo kinyume na taratibu na yanalenga kuzuia usafirishaji usio halali wa vijana wenye umri mdogo kutoka katika nchi zao.
Kutokana na ukatazwaji huo wa kusajili, endapo klabu hiyo ikimuuza Griezman haitopata mbadala wake.
Atletico Madrid itakubali Kumuuza Griezman endapo tu Manchester United Itakua tayari kutoa Dau la zaidi ya Shilingi Bilioni 247.
Manchester United imekua ikihangaika kutafuta mchezaji atakayecheza No 9 kuziba nafasi ya Zlatan Ibahimovic ambaye ameumia.
Imeelezwa kua endapo Manchester United itamkosa Griezman, chaguo la Kocha Jose Mourinho ni Romelu Lukaku (24) wa Everton au Alvaro Morata (24) wa Real Madrid.
Alexandre Lacazette ndiye mchezaji aliyekua anatumainiwa kuziba pengo la Antonio Griezman endapo angeondoka, lakini ndoto za Diego Simeon zimeonekana kuyeyuka baada ya katazo hilo la mahakama ya kisoka.
CHANZO: MANCHESTER UNITED KUFIKIRIA UPYA DAU LA ZAIDI YA TSH. BILIONI 247 KUMNUNUA GRIEZMAN