Man City na Liverpool ngoma yaisha kwa sare ya 1-1, Guardiola na Nunes warushiana maneno

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,628
6,294
ManchesterCity imeendelea kushika usukani wa Premier League kwa kufikisha pointi 29 licha ya kulazimishwa sare ya goli 1-1 katika mchezo dhidi ya Liverpool yenye alama 28 kwenye Uwanja wa Etihad, leo Novemba 25, 2023

Erling Haaland amecheka na nyavu upande wa City dakika ya 27 huku Alexander-Arnold akiisawazishia Liverpool dakika ya 80.

Mara baada ya filimbi ya mwisho Kocha wa City, Pep Guardiola na mshambuliaji wa Liverpool, Darwin Nunez walionekana kurushiana maneno huku chanzo kikiwa hakijajulikana.
 
Gunners from Northern London tutafurah zaid Kama tukixhnda mech ili tuxhke uxukan wa EPL
 
Sioni sababu ya kuendelea na matumizi ya VAR ligi ya EPL kwani matukio mengi yanaleta ukakasi,,
 
Liverpool walikuwa walazwa kwa goli
ManchesterCity imeendelea kushika usukani wa Premier League kwa kufikisha pointi 29 licha ya kulazimishwa sare ya goli 1-1 katika mchezo dhidi ya Liverpool yenye alama 28 kwenye Uwanja wa Etihad, leo Novemba 25, 2023

Erling Haaland amecheka na nyavu upande wa City dakika ya 27 huku Alexander-Arnold akiisawazishia Liverpool dakika ya 80.

Mara baada ya filimbi ya mwisho Kocha wa City, Pep Guardiola na mshambuliaji wa Liverpool, Darwin Nunez walionekana kurushiana maneno huku chanzo kikiwa hakijajulikana.
Mchezo wa jana naona Bahasha zilifanya kazi. VAR na Refa pamoja na washika vibendera walilamba bahasha....maana si kwa kuwaona vile Man City. Nahitaji team ishinde kihalali na si kuonewa. Jana wazi kabisa Refarii alikuwa kalamba bahasha. Lile goli lilikataliwa kwa kosa lipi? Wachezaji wa Liverpool waliunawa mpira ndani ya box la penalt mara mbili lakini Refarii hakujali kabisa. Hovyo kabisa.

Kwa upande wa pili..kocha wa Man City alipaswa kumwondoa Duke maana jana mpira ulikuwa umemkataa kabisa...na kiasi fulani alikuwa anachelewesha pia kusita kucheza mara nyingi.
 
Sioni sababu ya kuendelea na matumizi ya VAR ligi ya EPL kwani matukio mengi yanaleta ukakasi,,
Kweli kabisa, Like goli la Troussand lilikataliwa kwa sababu zipo? Nadhani Ligi Kuu Wana hasira na Arteta kwa sababu amegoma kunyamaza!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom