Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,713
- 13,464
Baada ya memba wa JamiiForums.com kulalamikia mchakato wa kuwaondoa Wananchi walio ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Mgori mamlaka zimejibu na kutoa ufafanuzi, soma hapa hoja ya Mdau - Watu wanaodhaniwa Askari wa Polisi na Maafisa Msitu wawapiga Wananchi, kuchoma moto makazi na mazao Wilaya ya Chemba na Ikungi
Maelezo ya TFS
Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Kanda ya Kati, Mathew Kiondo anafafanua: "Kinachofanyika ni maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan kuondoa wavamizi waliopo katika Msitu wa Mgori.
“Rais alipokuwa akiwasili Singida katika ziara akasema wakati akiwa anawasili aliona msitu mzuri lakini unaharibiwa, kwa tamko hilo maana yake ni maelekezo ya Mkoa na Wilaya.
"Kamati ya Ulinzi na Usalama ikatoa tangazo watu wahame katika Hifadhi ya Msitu wa Mgori, siku ya kwenda kupeleka tangazo hilo Wananchi waliovamia msitu huo wakawashambulia watu wa usalama akiwemo Mkuu wa Wilaya kwa kutumia mishale, mawe, rungu na nyinginezo.
"Baada ya kujipanga tukarejea na kwenda kufanya zoezi la kuwaondoa wavamizi hao, hatukutumia nguvu, kwa kuwa wao waliona tumeongozana na Watu wa Usalama, Askari wa FFU, Mgambo hawakufanya fujo, zoezi ni endelevu na litafanyika kwa siku 14.
“Tulichofanya tuliharibu makazi yao ya muda ambayo yapo ndani ya Msitu, wanafanya hivyo kujenga makazi ya muda kwa kuwa wanajua sio sehemu sahihi kwao.
“Kilichoharibiwa ni makazi yao lakini mazao, chakula na mifugo vyote havijachukuliwa wamekabidhiwa na kutakiwa kurejea kwenye vijiji ambavyo vipo kando ya Misitu.
"Lazima tuwe na ubinaadamu, kisheria ilitakiwa hata mifugo yote tuitafishe lakini tuliwaachia waondoke nayo.
“Pamoja na hivyo zipo taarifa zisizo rasmi kuwa baadhi ya mifugo ambayo inaingizwa ndani ya Hifadhi ni ya watu wenye nafasi katika siasa, hivyo hawa Wananchi wanatumika tu.”