KERO Mamlaka ya Maji Singida (SUWASA) mnatuumiza sana Wananchi, bili mnazoleta haziendani na uhalisia

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mliogwa

Member
Jun 6, 2024
33
32
Salaam Wanajukwaa,

Naomba kero yangu ifike kwa waziri Jumaa Aweso kilio chetu Wananchi wa Singida, SUWASA inatuua.

SUWASA inatukandamiza, inatuonea, bili za maji za huku kwetu ni mitaji ya Watu huko SUWASA, haiwezekani bill zinakuja bila mpangilio.

Hivi majuzi jirani yangu alikuwa akilalamika kuwa maji nyumbani kwake hayatoki na hata alipoenda SUWASA aliambiwa watakuja kurekebishq mwezi ukaisha hawajakqnyaga. Hafla akashangaa analetewa bili ya ya Shilingi 15,000.

Mimi nilisafiri miezi miwili sipo nikiwa huku niliko nimetumiwa bili ya 20k wakati huohuo nyumbani hamna mtu.

Naishi mwenyewe. Nyumba na bomba limefungwa. HII SI SAWA...

Leo hii mwenzetu naye analalamika kuwa wakati TARURA wanatengenezq barabara walikata mabomba. Wamekaa mwezi mzima maji yakiwq hayatoki ndani yameanza kutoka Alhamis iliyopita.

Kuanzia septemba hana maji, leo kaletewa bili ya Sh. 10,500.

TUNAOMBA TUELEWESHWE mnafanyaje kupiga hesabu matumizi ya unit zenu? Maana huu mnaofanya ni uonevu.

Pia soma ~ Singida: Wakazi wa Sabasaba Singida Hatuna maji wiki ya pili sasa
 
Hawa idara ya maji ni majizi nchi nzima, mko watu 2 ila bili ni elfu 40 Kwa mwezi! Rubbish kabisa!

Hata hapa Arusha ni hivyo hivyo! A failed country!
 
Kibaya zaidi ni mgao mkali wa maji kiangazi hiki, maji hayatoki siku mbili hadi tatu, na yakitoka ni masaa machache tu yanakatika. Wananchi wanachota maji kwa kuvizia siku ya kutoka.
 
Omba ufungiwe zile mita za malipo kabla (mita kama za LUKU)
 
Salaam Wanajukwaa,

Naomba kero yangu ifike kwa waziri Jumaa Aweso kilio chetu Wananchi wa Singida, SUWASA inatuua.

SUWASA inatukandamiza, inatuonea, bili za maji za huku kwetu ni mitaji ya Watu huko SUWASA, haiwezekani bill zinakuja bila mpangilio.

Hivi majuzi jirani yangu alikuwa akilalamika kuwa maji nyumbani kwake hayatoki na hata alipoenda SUWASA aliambiwa watakuja kurekebishq mwezi ukaisha hawajakqnyaga. Hafla akashangaa analetewa bili ya ya Shilingi 15,000.

Mimi nilisafiri miezi miwili sipo nikiwa huku niliko nimetumiwa bili ya 20k wakati huohuo nyumbani hamna mtu.

Naishi mwenyewe. Nyumba na bomba limefungwa. HII SI SAWA...

Leo hii mwenzetu naye analalamika kuwa wakati TARURA wanatengenezq barabara walikata mabomba. Wamekaa mwezi mzima maji yakiwq hayatoki ndani yameanza kutoka Alhamis iliyopita.

Kuanzia septemba hana maji, leo kaletewa bili ya Sh. 10,500.

TUNAOMBA TUELEWESHWE mnafanyaje kupiga hesabu matumizi ya unit zenu? Maana huu mnaofanya ni uonevu.

Pia soma ~ Singida: Wakazi wa Sabasaba Singida Hatuna maji wiki ya pili sasa
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) ina utaratibu wa kusoma Dira kwa wateja wake tarehe 1 hadi 7 ya kila mwezi.

Usomaji mita huwa ni shirikishi baina ya SUWASA na Mteja na wateja wote wameelimishwa kuwa Mita ikisomwa, meseji ya usomaji (SMS) huingia kwa mteja (katika simu ya Kiganjani) ili afanyale uhakiki ya kilichosomwa katika Dira.
Iwapo mteja ataona kuna tofauti ya meseji ya usomaji na Dira inavyoonesha, apige simu ya Bure ya SUWASA ili hatua zichukuliwe kwa haraka. Katika taarifa kadhaa za namna hii ni maeneo ya wateja ndio yamebainika kuwa na shida za uvujaji na kishauriwa kifanya maboresho. Wateja wanashauriwa kutoa ushirikiano kwa SUWASA ili huduma iendelee kuwa Bora.
 
Back
Top Bottom