Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 539
- 756
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeendelea kung'ara katika uwanja wa usimamizi wa fedha za Umma. Katika hafla ya tuzo iliyofanyika usiku wa tarehe 29 Novemba 2024, DCEA ilitangazwa mshindi wa kwanza tuzo ya umahiri katika utayarishaji bora wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2024 katika kipengele cha Taasisi za serikali zinazojitegemea (Independence government agency).
Akizungumza wakati wa kupokea tuzo hiyo kwa niaba ya Kamishna Jenerali, Kamishna Hussein Mbanga alisema kuwa ushindi huu wa mara kwa mara unadhihirisha uadilifu wa DCEA katika kuhakikisha kuwa fedha za Umma zinazotumiwa katika kupambana na tatizo la dawa za kulevya zinatumika kama inavyotakiwa.
Kwa upande wake, Mhasibu Mkuu wa DCEA, CPA Stephen J. Dalasi alisema kuwa ushindi huu ni ushahidi kuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amepitisha kuwa hesabu za Mamlaka ni safi kabisa. Aliongeza kuwa utendaji huu bora utakuza zaidi imani ya Umma kwa DCEA katika usimamizi wa fedha.