Mkuu, mimi ni mwana JF na mdau wa sayansi hii ya hali ya hewa, hivyo naomba nitumie nafasi hii kutekeleza lengo mojawapo la mtandao wetu pendwa wa JF la kuelimishana.
Kama hoja imeanzia mvua za jana na leo kwa mikoa ya pembezoni mwa bahari ya Hindi basi kuna taarifa ilitoka kabla ya hiyo update uliyo iweka wewe. Attachment hii hapa.
Kuhusu mafuriko ya mwezi machi Dar es Salaam, kwanza niseme kwa Dar es Salaam sio mara zote mafuriko yanasababishwa na mvua kubwa, kama unavyo fahamu mji huu umejengwa bila mpangilio mzuri hivyo njia nyingi za maji zimezibwa, mafuriko kwenye mkoa huu sio kipimo kizuri sana cha ubora wa utabiri. Kama kazi zako za kila siku zinategemea utabiri wao moja kwa moja basi nikushauri wasiliana nao uwe unapata taarifa kwa njia ya simu na mitandao.
Kuhusu vifaa gani hutumika kutabiri hali ya hewa, jibu lake hakuna vifaa vinavyo tumika kutabiri hali ya hewa. Vipo vifaa ambavyo hutumika kupima taarifa za hali ya hewa kama mvua, hali joto n.k. Utabiri wa hali ya hewa ni matokeo ya vitu vingi kuanzia ukusanyaji wa taarifa za hali ya hewa (vipimo), analysis ya mifumo inayo tawala hali ya hewa katika eneo letu na dunia kwa ujumla n.k.
"Rain Gauge ni kifaa cha bei rahisi sana kupima kiwango cha mvua".
Hapa mkuu kama nimekuelewa sawa lengo lako ni kuhusisha ubora wa kipima mvua, bei yake na ubora wa utabiri. Kama ni hivyo basi jibu ni kuwa, kipima mvua hakina uhusiano na ubora wa utabiri wa mvua, kwasababu mvua ni matokeo.
Ubora wa utabiri wa mvua unaweza kuhusishwa na ubora wa vipimo vya hali joto, mgandamizo wa hewa na upepo n.k.
Taarifa za TMA katika miaka ya hivi karibuni zimekuwa na ubora unaoridhisha ingawa pia kuna nafasi ya kufanya vizuri zaidi. Kikubwa kwa walaji ni kuongeza umakini katika usikilizaji na ufatiliaji wa taarifa hizo.
Ufafanuzi huu ni wangu kama mwana JF na mdau wa sayansi hii ya hali ya hewa na sio majibu ya TMA.