Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,318
- 4,646
Mamlaka tueleze kama kuna utaratibu unaruhusu kuendesha gari hisiyo na namba tunapata hofu tunapokutana nazo
Kumekuwepo na gari ambazo zimekuwa zikiendeshwa barabarani bila kuwa na ‘pleti namba’ jambo ambalo kulingana na uwepo wa taarifa za uwepo wa matukio ya utekaji pamoja na visa vya watoto kudaiwa kupotea, inabua hofu.
Hofu hiyo hasa inatokana na baadhi ya Watu kuwa na mitazamo kuwa wahusika wenye magari hayo wanaweza kutenda tukio ovu na wasitambulike kwa uharaka.
Mimi ni Mkazi wa Tandale kwa zaidi ya wiki imekuwa ikipita pita gari ambayo haina namba jambo ambalo linanipa hofu mimi binafsi pamoja na wengine lakini tunakosa kuchukua hatua zipi.
Naomba mamlaka zitujuze kwamba kuna taratibu zozote za Kisheria ambazo zinatoa ruhusa kwa Mtu au Watu kutembea na gari isiyo na namba.
Tunajua kuna wakati inaweza kutokea dharura namba ikatoka, lakini hakuna njia mbadala inaweza kutumika hata kuweka namba za dharura hususani kipindi kama hiki ambacho Watu tuna hofu kutokana na wimbi la matukio yanayohusisha vyombo vya aina hiyo (magari yasiyo na namba au yenye namba zenye mashaka).
Kwa mazingira ya aina hiyo inaweza kuwafanya Wananchi wakataka kujichukulia Sheria mkononi jambo ambalo uenda likaja kuwa na athari zaidi, japo nabakia kujiuliza wanaofanya hivyo wanajiamini kiasi gani na hali iliyopo kwa sasa au hawana taarifa dhidi ya matukio ambayo yamekuwa yakiripotiwa hivi karibuni.
Tutakumbuka wiki kadhaa zilizopita ilidaiwa kuonekana gari nyeusi hisiyo na plate namba maeneo ya Mburahati Shule, kilichotokea Wazazi walikimbilia Shuleni kutaka watoto wao jambo ambalo liliibua taharuki, licha ya taarifa ya Jeshi la Polisi kudai madai hayo hayakuwa na ukweli.