GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,443
- 120,800
Haiwezekani katika Vituo vyote vya mabasi ( Daladala ) gharama ya huduma ya Choo ni kati ya Tsh 200/ hadi Tsh 300/ tu lakini katika Kituo cha basi cha Mbezi mwisho iwe unaenda Kukojoa au Kukimbika au Kuoga bei ni ile ile Tsh 500/ huna kajenge Choo chako.
Gharama hii inawatesa sana Wazee hasa akina Bibi na Babu ambao binafsi nimekuwa nikiwaona mara kwa mara wanavyoteseka hapo na hiyo gharama kubwa ya huduma ya Choo hali ambayo imefanya hadi Watu wengine ( abiria ) kuamua kuwasidia na kuwalipia ili Wazee hao na wao wawahi Vyooni kufanya yao.
Ili kuonyesha kwamba Watu wengi wamekereka na gharama hii kubwa sasa Watumiaji hao vya hivyo Vyoo sasa wamebuni mbinu mpya ya kuwakomoa wale wahudumu wa hivyo Vyoo na hasa upande wa Wanaume ambako kiukweli Mtu akitoa hiyo Tsh 500/ anachoenda kukifanya mule ndani ni zaidi ya hiyo Tsh 500/ kwani wapo ambao huamua kukojoa katika masinki ya maji lakini wapo ambao sasa huamua kabisa kuachia Vinyesi vyao ( Kukimbika / Kunya ) mule ndani Sakafuni huku wengine wakiviachia na kuvipaka ukutani kwa kufanya Graffiti zao za Kutukuka.
Tafadhalini Mamlaka husika hebu liangalieni hili la gharama hii kubwa ya Choo cha Kituo cha Mabasi cha Mbezi mwisho angalau basi iwe Tsh 300/ kwani kwa kuendelea Kwenu Kukomaa nayo mnawapa sana wakati mgumu Wahudumu wenu hapo ambao Kiukweli wanakoma na jinsi nasi pia tunavyowakomoa kwa kukojoa hovyo mule ndani na kuacha Mikimba yetu iliyoyukuka wazi wazi kwa hasira.
Bora sisi wengine Wajanja tukishashuka hapo na kama tumebanwa na Kojo au Nnya huwa tunazunguka kwa nyuma kule kwa chini ambako huwa kuna Baa nyingi na tunachokifanya ni kujenga Urafiki wa ghafla na wale Wahudumu na kujifanya tunataka huduma pale ya ama Chakula au Vinywaji kisha tunajifanya tunaulizia Vyoo na tukienda huko tunamaliza yetu na tukirudi tunajifanya tunaongea na Simu au tumepigiwa Simu za dharura na kuondoka pale ili mradi tu tukwepe kulipishwa chochote au kupata huduma pale. Sasa ni wangapi wana huu Ujanja?
Lifanyieni Kazi hili upesi kama siyo haraka sana kwani Wananchi hasa Abiria wa Kituo cha Mbezi mwisho wanateseka na hii gharama yenu cha Choo ya Tsh 500/. Natumai mtatupa ushirikiano katika hili.
Nawasilisha.