Mamlaka husika mnatambua jinsi wafanyabiashara maduka ya rejareja wanavyoibiwa sukari, ngano na sembe katika maduka ya jumla wilayani Bunda?

Mjukuu wa kigogo

JF-Expert Member
Sep 19, 2023
441
1,083
Wanajamvi wakati tunaendelea kumuona Makonda akiendelea kuuwasha moto na kuendelea kuwa man of the match kuna kitu nimekibaini....!

Maduka mengi ya jumla(wholesale) hapa wilaya ya Bunda yananyonya sana wafanyabiashara wadogo wadogo(wa rejareja),ila mbinu wanayotumia ni kali sana!

Wanachokifanya kama mfuko wa kg.50 unauzwa let say 126000 watakuuzia Kwa 124000 au 123000. Kiuhalisia hapa unakuta kg2 mpaka tatu zimepigwa bomba(zimechotwa kitaalamu).Bahati mbaya mfanyabiashara mdogo hupenda duka lenye unafuu zaidi na mbaya zaidi 99%ya wafanyabiashara wa rejareja hawana spring balance, yeye ni kununua,kuita pikipiki na kukimbiza mzigo dukani tayari kabisa kuchukua maokoto toka kwa wateja!Mbaya zaidi naye akiona kauziwa kwa bei ya chini naye atapunguza bei ya kg!Hali hii pia ipo katika viroba vya sembe na ngano!Hali ni mbaya sana!

Bahati mbaya zaidi wauzaji wa rejareja huwa ni nadra kupiga hesabu anachofurahia wateja kujaa mwisho wa siku biashara inakufa maana ni hasara juu ya hasara!

Mamlaka husika chukueni hatua mapema kunusuru wajasiriamali wadogo wadogo ambao ndio walipa Kodi wakubwa katika nchi hii.

Jaribuni kufanya msako wa kustukiza!

Hebu anzeni na stoo ya MJENG
 

Attachments

  • FB_IMG_1699971615085.jpg
    FB_IMG_1699971615085.jpg
    43.4 KB · Views: 8
Back
Top Bottom