Mamia ya nyati wamekufa maji katika mto wa mpakani kati ya Botswana na Namibia

BuletAngle

JF-Expert Member
Apr 15, 2017
688
556
Mamia ya nyati wamekufa maji katika mto wa mpakani kati ya Botswana na Namibia.



CaptionWenyeji waliamkia mamia ya nyati waliyokufa katika mto Chobe


Mamia ya nyati wamekufa maji katika mto wa mpakani kati ya Botswana na Namibia.
Uchunguzi wa awali unaashiria kuwa wanyama hao walikuwa wakifukuzwa na simba wakakimbilia mtoni.
Mmiliki wa hoteli karibu na mto huo ameiambia BBC kuwa nyati hao walikwama kwasababu kingo za mto zilikuwa juu sana
hali iliyowafanya wanyama hao kukanyagana hadi kufa.


Mamlaka nchini Botswana inakadiria kuwa karibu nyati 400 walikufa katika kisa hicho.
Watu wanaoishi karibu na mto huo walijipatia kitowea cha nyama nyama na kujipelekea nyumba .
Simone Micheletti, ambaye ni mmiliki hoteli moja upande wa mpaka wa Namibia, anasema idadi ya wanyama hao ilikuwa kubwa kupita kiasi.





Bwana Micheletti ameiambia BBC kuwa simba walisikika wakinguruma sana usiku wa Jumanne.
''Niliposhuka mtoni asubuhu ya Jumatano niliona mamia ya nyati wakiwa wamekufa.


Ameongeza kuwa usiku wa Jumanne ulikuwa na mawingu ya mvua ambayo huenda ilikinga mwangaza wa mwezi ambao hutumiwa sana na wanyama nyakati za usiku.
Wizara ya mazingira ya Botswana imetoa taarifa kuelezea kuwa hiki si kisa cha kwanza cha wanyama kufa maji katika mto Chobe.
Lakini bwana Micheletti amesema idadi kubwa kama hiyo ya wanya kufa maji haijawahi kushuhudiwa.




 
Nyati 400 kuwakimbia simba?
Labda kama hao walikuwa 800
 
Msaada:

Nini tofauti kati ya Nyati, Mbogo na Nyumbu
 
Nyatu huwa wananfata mkubwa wao. Yan ni kam vijna wa lumumba..wenyewe ni ndyo mzee hawajiongezagi. Kubwa lao akiingia hata kwenye shimo na wenyewe ivyo ivyo wanajitosa bila hata kuangalia nyuma au pembni
 
tatizo lako ni kubwa tena kubwa sana..
usifikiri kila kile unachowaza ni sahihi wakati wote...
niambie basi maandiko gani yanaruhusu kula mizoga..
Tunarudi pale pale, hayo maandiko kaandika nani.?? Tofauti ya ww usie kula kibudu na anaekula vibudu ni nn.?? Tuache kushikiwa akili. Kama mnyama hajafa kwa ugonjwa analiwa kama kawaida, we endelea tu kushikiwa akili watu wanatafuna minofu tu uko
 
hata shule inaonekana hujaenda kula mzoga ni hatari kwa afya...
wanakula hizo nyama wana uroho wa nyama ndio wanakula hizo mizoga...
ukiwa unakula nyama kwa ukawaida uwezi kuokota mizoga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…