LIVE Mamelodi Sundowns 0 - 0 Al Ahly SC | CAFCL | Semi-Final | 1st Leg | Loftus Versfeld Stadium | 19-04-2025

Live coverage on JamiiForums

uran

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
10,573
16,225
πŸš¨π™‚ 𝘼 π™ˆ 𝙀 𝘿 𝘼 π™”πŸš¨
⚽ Mamelodi Sundowns vs Al Ahly FC
πŸ“† 19 April
⏰ 16H00
🏟 Loftus Versfeld Stadium
1000064025.jpg


Mtanange mkali sana huu!
Mimi nitakuwa tayari kuwapa updates zote muhimu kwa Siku ya leo.

Binafsi nawatakia Masandawana Kila la heri.

VIKOSI VINAVYOANZA LEO.
Mamelodi Sundowns
1000064565.jpg


Al Ahly
1000064564.jpg


Updates...
15H57
Timu zimeingia uwanjani tayari kwa kuanza Mtanange huu wa kukata na shoka.
Uwanja bado unaonekana na gaps za kutosha,
Huko Afrika Kusini ni saa tisa kasoro sasa.

Dk 0.49"
Emam wa Al Ahly anapata injury kidogo baada ya kublock vibaya mpira, ametoka nje kidogo kupata matibabu.

DK 05'
Mpira unaendelea sasa umiliki kwa Masandawana, huku Al Ahly wakionekana kucheza defensive game.
Wanaenda kwa tahadhari sana.

DK 07'
Al Ahly anapata kona ya kwanza, inapigwa hauleti madhara yoyote kwa Mamelodi.
Game on...bado mpira ni wa kukimbizana.

DK 10'
Mamelodi wanafanya shambulizi kali sana kwenye lango la Ahly lakini linaishia na goal kick.
Game On
0-0

DK 13'
Umiliki ni kwa Mamelodi sasa wanapiga pasi nyingi hapa kati na kujaribu penetrative passes zinazowafanya Al Ahly waongeze umakini.
Asimilia kubwa wako nyuma.
Game On
0-0

DK 17'
Mamelodi wanamiliki mpira kwa kiasi kikubwa sasa.
Wanafanya mashambulizi kwa kupiga mashuti ya mbali, yanakuwa off target, hii itasaidia kwasababu Al Ahly wamejaa golini kwao.
Game On
0-0

DK 22'
Mpira unaendelea, kuna mahali Mamelodi wanafika ila wanaoshia kupoteza.
Mudau mipira mingi inapotelea kwake.
Kuna mchezaji mmoja wa Al Ahly kalamba nyasi hapa.
Wanapata Free Kick nje kidogo ya 18.
Inapigwa inapokelewa na kichwa inatoka nje.
Goli kick
Game On
0-0

DK 27'
Mpira umiliki kwa Al Ahly sasa wanajaribu na wao kutembea kwa pasi ndefu ndefu, ila hawadanikiwi kufanya mashambulizi ya maana.
Mpira unarudi kwa Masandawana kama kawaida yao wanacheza maeneo ya kati sana .
Game On
0-0

DK 36'
Mamelodi wanapata kona wanapiga wala haileti madhara yoyote kwa Al Ahly.
Game on
0-0

DK 45'
Zimekamilika nyongeza ni 2'
Game on
0-0

Half Time.
Mamelodi Sundowns 0 - 0 Al Ahly.

=======================
Updates 2nd Half.

DK 52'
Mamelodi wanapata free kick nje kidogo ya 18.
Inapigwa inawababatiza Al Ahly wanaokoa.
Wanapata free kick nyingine eneo lile lile.
Ni nje kidogo ya 18.
Inapigwa inaokolewa hapa na walinzi wa Al Ahly, kipindi cha pili kimeanza kwa kasi kidogo.
Kipa wa Al Ahly yuko chini mpira unesimama kidogo
0-0

DK 58'
Wachezaji wa Al Ahly wanalalamika kuwa mpira ulichezwa kwa mkono kwenye lango la Mamelodi.
Refa anapeta, picha za marejeo hazionyeshi kama mpira ulishikwa
Game On
0-0

DK 62'
Mamelodi wanafanya sub mbili.
Shelulie Out
Mathews Out
Ryanes Inn
Game on
0-0

DK 65'
Kuna mchezaji wa Al Ahly yuko chini, inaonekana wanapiteza muda.
Mpira umesimama kwa muda
0-0

DK 69'
Modiba wa Mamelodi anapewa kadi ya Njano.
Wakati huo huo wanafanya mabadiliko.
Adams out

DK 70'
Gradisar wa Al Ahly anatupia goli linakataliwa.
Offside

DK 72'
Mchezaji mwingine wa Al Ahly yuko chini
Mpira umesimama kimama kidogo
0-0

DK 74'
Game On
Timu zinashambuliana kwa zamu,
Al Ahly wanafanya ulinzi madhubuti, wakati Masandawana wanafanya mashambulizi hafifu sana
0-0

DK 77'
Allende wa Mamelodi anapatiwa kadi ya njano kwa kucheza rafu dhidi ya Al Ahly.
Inapigwa free kick nje kidogo ya 18 kuelekea kwa Masandawana inaishia kwenye mikono ya Kipa.
Game On
0-0

DK 80'
Bado hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.
Itabidi makocha wabadilishe mbinu
0-0

DK 86'
Mamelodi wanapata kona ila inakuwa tasa.
0-0

DK 89'
Al Ahly wanafanya Sub 3.
Game on
0-0

DK 90'
Nyongeza ni Dakika 7
Game on
0-0

DK 90+2'
Al Ahly wanapata goli, ila inaonekana mchezaji aliyefunga alikuwa ameotea.
Game On
0-0

DK 90+5'
Mchezaji wa Al Ahly anapatiwa yellow card kwa kucheza rafu.

Full time
Mamelodi 0 - 0 Al Ahly.
Imeisha Hii.
 
Mamelod nilikua nawakubali sana ila tangu waliposhindwa kuikamilisha ile task mpaka kufikia penati shootout na wale vitoga kuanzia pale nikawaachia laana.

Na kufuatia tukio la juzi hapo la kufungwa goli dhidi ya Esperence halafu wakafanya ufuska kulikataa kwa sababu za uongo ndio inazidi kunipa midadi ya kuendelea kuichukia.

Huu umbali wote tusingefika, tupo hapa kwasababu ya uzembe wao. Iwapo wangepiga Gongowazi ndani ya dakika 90 haya yote yasingetokea.
 
Naomba Masandawana wafanye kama walichofanya Gunners, furumusha timu zote zilizojiwekea ufalme kwenye kutwaa makombe ya klabu bingwa karibu kila msimu, yaani hadi michuano inapoteza mvuto maana mwisho wa siku bingwa anajulikana ni yule yule wengine mnakuwa kama wasindikizaji tu
 
Naomba Masandawana wafanye kama walichofanya Gunners, furumusha timu zote zilizojiwekea ufalme kwenye kutwaa makombe ya klabu bingwa karibu kila msimu, yaani hadi michuano inapoteza mvuto maana mwisho wa siku bingwa anajulikana ni yule yule wengine mnakuwa kama wasindikizaji tu
All the best, Masandawana...
 
Mamelod wazembe flani,pia inakuzwa.Wakishindwa kupata ushindi mkubwa kwao leo ndo kwaheri.

Mwarabu akija kwako pigaaaa za kutosha ili kwake ukafulukute tu
Na waarabu kwa kulijua hilo ndio maana wakianzia ugenini wanapaki tu basi walau wapate draw ya bila bila ili wakakumalize kwao
 
Back
Top Bottom