Mambo yasiyofaa kufanya unapokwenda Maabara kupima Hospitali za Serikali

pakamwam

JF-Expert Member
May 28, 2013
516
653
1. usimpangie mtaalam akupimeje. mara nyingi wagonjwa wanaokuja hospitali vipimo huombwa na daktali aliyekupokea, mtaalam wa maabara ana[otaka kukupima unatakiwa kumpa ushirikiano

2. una haki ya kuelezwa aina ya kipima unachochukuliwa na pia una haki ya kukaa kutoa kipimo hicho( patient consent)

3. ni kosa kubwa kumlazmisha mwanasayansi wa maabara au technician au technologist kutoa majibu kwa muda unaotaka wewe. unapotolewa kipimo uliza turn around time ya kipimo hicho ni muda gani. yeye atakueleza turn around time na usimshurutishe kutoa majibu kabla ya hapo. kumbuka kumpa mtu majibu sio ishu maana unaweza kuandika tu, lakini kumpa mtu majibu yenye uhakika na usahihi inahitaji utaalam na patience

4. inaweza kutokea mtaalam akaomba ulete au uchukuliwe kipimo kingine kwa maana uchomwe sindano tena au kuleta mkojo, choo, makohozi, tissue au maji maji ten, ni kawaida na ukiona anafanya hivyo ujue ni mwaminifuna inawezekana kaona kitu kisicho cha kawaida kwa hiyo anataka uhakika zaidi

5.epuka kufokea au kukwaruzana na wataalm hawa kutokana na presha ya ugonjwa au mgojwa wako, zoezi la kutafuta ugonjwa linahitaji umakini mkubwa sana ndio maana mtu yeyote asiyehusika haruhusiwi kuingia maabara

6. majibu sahihi yaweza kuwa positive, negative, inderminate na parameters zingine, kila jibu utakalopata maabara lina umuhimu katika matibabu.

mengine nitaendelea kesho kuhusu elimu ya upimaji na vipimo kwa rais wema sana sana jf members
wenu katika ujenzi wa taifa
 
Kaushauri kangu hasa huko private. Huwa wanajaza mavipimo ili wakupige nying. Kwahiyo ata hili tusiseme?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…