mmmuhumba
JF-Expert Member
- Nov 8, 2017
- 493
- 478
Mahusiano yana raha zake na shida zake, ila kuna kitu cha kujifunza na kukiepuka mwanamke na mwanaume. Kila jinsia katika mapenzi huwa na mategemeo yake na hivyo ujipambanua pindi tu unapotongoza ama kutongozwa unapata kujua mtu husika kama anafaa au lah, na hukupa mwanga wa kufanya maamuzi sahihi ya kuwa naye au kutokuwa naye.
Mambo haya mwanaume hukosea na kumfanya mwanamke aone hana haja ya kuwa naye kimapenzi:
Kujisifia kupita uhalisia. Wapo wanaume wanapotongoza wanawake na kutoka nao kwa mara ya kwanza, huongea mengi ya kujipambanua kihadhi, kiutafutaji, kimapenzi na kumjua mwanamke mpaka inakera na kuonyesha ni muongo na muendekeza ngono. Wanawake timamu hawapendi kudanganywa. Iwe ni tajiri ama maskini kuzidisha sifa ni sumu.
Kutaka vitendo vya mapenzi hata kabla hajakubaliwa. Kama kumbusu, kumshika shika, kumkumbatia, kumtia vidole katika nyeti zake na mengine ujuayo, hivi kwa mwanamke huwa ni kama udhalilishaji. Kwa mara ya kwanza na akupe ruhusa kufanya vyote, hii ni hulka ya aina fulani za wanawake ambao wao ni maji mara moja wameiva.
Kuonyesha chuki na wanawake. Usimtongoze mwanamke na kuonyesha hasira zako za kutendwa na kutokuwa na imani na wanawake. Lazima utambue unapotaka kuanzisha mahusiano hata kama umetendwa na moyo wako una matobo kama neti, hupaswi kuonyesha chuki wala kukosa imani naye. Wanawake huogopa mwanaume anayechukia jinsia yao.
Kuwa na mkono mfupi. Mwanaume ili uonekane unajali na huna choyo, usiwe mgumu katika matumizi pale unapomtoa mahali kwa mara ya kwanza unapomtongoza kwa vijizawadi, vocha, vibaiti na hata kumpa fedha ya matumizi, uona wewe unajali. Wanawake wanapenda wanaume mabahiri kimaisha ila siyo kimapenzi, hutambua hutoweza kumhudumia wala kusaidia familia yake bali utamfubaza tu.
Kutokujiamini. Kujiamini huonyesha wewe ni mwanaume mwenye msimamo, ila unapokuwa unatongoza, upo kwenye mahusiano au umetoka naye mahali lakini unashindwa kusimama kama mwanaume, hilo ni tatizo. Mwanamke huhitaji mwanaume atakayekuwa tayari kumlinda na mwenye msimamo na anachokiongea.
Kuzungumzia sana x wako/zako. Siyo kila mwanamke hupenda kusikia hadithi za wanawake uliyokuwa nao kwenye mahusiano kabla yake, baadhi ya maneno huweza kumuumiza, kumtusi, kuonyesha yeye hakufai kwa kujilinganisha kupitia hadithi ya huyo x wako. Lakini pia unapoeleza unaweza onyesha hisia kuwa wewe akili yako bado ipo kwa x wako.
Kutoonyesha msimamo na ndoto zako za maisha. Wanaume wengine hata kama wamejikamilisha kimaisha, lakini katika mazungumzo yao hawaonyeshi wanawawazia nini wanawake zao husika katika maisha yao. Na wanaume wa hali ya kawaidia kukosea kuzungumzia ndoto zake na matarajio yake ya maisha akiwa na huyo mwanamke. Mwanamke huona raha kushirikishwa katika ndoto na maisha ya mwanaume, ndiyo maana wanawake wapo radhi kujenga ndoto za wanaume zao kuliko zao.
Kumlinganisha. Unapompeleka mahali husika, mwanamke hujipima hadhi, mazungumzo yako ukikosea na kumlinganisha na mwanamke mwingine ama mama yako ni bora kuliko yeye ilo ni tatizo. Ubinafsi katika mapenzi upo, kumsifia yeye kama yeye ndiyo hutakiwa, watu wengine waweke pembeni.
Kutokuwa tayari naye kimaisha. Yuko mwanaume anatongoza ila hayupo tayari kulea mimba japo anataka apewe ngono, hayupo tayari kumuoa ila unataka penzi lake na kumsifia mzuri. Mwanamke asiyemuoga wa maisha hawezi kubali kuwa chombo cha starehe.
Ni wazi katika mapenzi hakuna mwanamke wala mwanaume anayeingia katika mapenzi kwa lengo la kutaka kuteseke zaidi kutafuta raha. Mapenzi ni pambe na siyo pombe, tena ile ngumu kumeza. Kwa mwanamke yeye ni kiumbe wa kubembelezwa hata awe na mafanikio namna gani, raha yake ni kumpata mwanaume atayeweza kumpetipeti na kumuelewa kama mtoto.
#imarika#
#mnogeshe umpendae#
Na mmmuhumba.