Mr George Francis
JF-Expert Member
- Jun 27, 2022
- 234
- 366
CHUNGU na TAMU katika NDOA ndio maisha yenyewe. Tusingeweza kuijua RAHA kama kusingekuwepo na KARAHA. Nyakati ngumu katika maisha huwa zinakuja na kuondoka lakini baada ya yote, FURAHA inapaswa kudumu milele.
CHUNGU katika ndoa ni kawaida kutokea, lakini TAMU inapaswa kutawala maisha yote ya ndoa hadi mwisho wa uhai. Mwenyezi Mungu, tangu mwanzo anamuumba mwanadamu aliona sio vyema ADAMU kuishi peke yake, akamuumba na EVA.
Pamoja na changamoto zilizojitokeza hadi kufukukuzwa bustani ya EDEN, lakini ADAMU na EVA waliendelea kuishi pamoja na kufurahia TAMU ya maisha ya mume na mke.
TAMU katika NDOA inatengenezwa na CHUNGU katika NDOA inasababishwa.
Yafuatayo ni miongoni mwa mambo yanayochangia kuwa na ndoa TAMU na yenye FURAHA.
(i) UPENDO WA KWELI
Upendo wa kweli ndio nguzo muhimu katika maisha ya ndoa. Upendo unaweza kupelekea mume au mke kuchukuliana madhaifu yao na kuendelea kuishi kwa furaha na amani.
Neno la Mungu linasema,
"Zaidi ya hayo yote jivikeni UPENDO, ndio kifungo cha ukamilifu."
Wakolosai 3:14
"Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika."
1 Wakorintho 13:8
(ii) UVUMILIVU WA KWELI
Usijifanye kama unaweza kuvumilia hali ya kuwa kuna mambo yako mengine unayafanya nyuma ya pazia.
Katika maisha ya NDOA kuna nyakati mtapitia magumu na kuna nyakati utayaona wazi madhaifu makubwa ya mwenza wako.
Lakini katika yote hayo, unapaswa kuvumilia magumu hayo na madhaifu hayo ya mwenzi wako. Shirikiana na mwenzi wako katika kutatua magumu hayo au madhaifu yake yanayoweza kurekebishika.
Jizuie kuwa na hasira, kupigana ama kudharirishana.
Neno linasema,
"Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji."
"Mithali 16:32
(iii) MAWASILIANO MAZURI
Zungumza na mwenzi wako marakwamara tena kwa lugha nzuri ya staha. Maneno mazuri ya mahaba yanaimarisha upendo lakini maneno mabaya yanavunja moyo wa mtu na yanaweza pia kuvunja mahusiano na ndoa kusambaratika.
Chunga sana maneno unayozungumza na mume/mke wako usije ukaumiza hisia zake na kumfanya apoteze upendo kwako.
Neno linasema,
"Azuiaye maneno yake ni mwenye maarifa; Na mwenye roho ya utulivu ana busara."
Mithali 17:27
Hata panapotokea changamoto, zungumzeni wenyewe na kunyamaza. Msiwe wepesi kuyatoa nje mambo yenu ya ndani, hapo mtakaribisha CHUNGU katika ndoa.
Neno linasema,
"Mwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia."
Zaburi 4:4
(iv) HESHIMA YA KWELI
Kuwa na heshima kwa mwenzi wako na sio kuwa na nidhamu ya woga. Mfanye mume/mke wako aone kuwa unatambua thamani yake.
Usimtendee kile ambacho hata wewe usingependa kutendewa bali mtendee kile ambacho hata wewe ungependa kutendewa.
Kila mmoja na atimize majukumu yake na kutimiza hitaji la mwenza wake ili kila mmoja ajihisi kuheshimiwa na hiyo ndio TAMU n furaha ya NDOA.
(v) UAMINIFU WA KWELI
Tengeneza uaminifu kati yenu. Jengeni hali ya kuaminiana. Usaliti unaleta CHUNGU katika NDOA.
Usijifanye kama unamuamini bali muamini kweli.
"Bata ukimchunguza sana huwezi kumla."
Sio kila saa unakagua simu yake, au akiongea tu na mtu tayari unahamaki eti ni mpenzi wake.
Ndugu yangu tambua kuwa lawama za marakwamara zinapunguza radha ya mapenzi na mwishowe zinaweza kuvunja mahusiano au ndoa yenu.
(vi) MSAMAHA WA KWELI
Katika maisha ya mahusiano ya aina yoyote hususani maisha ya ndoa kugombana au kupishana kauli na kutofautiana mitazamo ni jambo la kawaida lakini isiwe kwa kiasi kile cha kupitiliza.
Ijapotokea mambo kama haya kubali kukaa chini na kumaliza tofauti zenu na kusameheana. Usijifanye kama umesamehe bali toa msamaha wa kweli.
Neno linasema,
"Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,
Mkichukuliana, na KUSAMEHEANA, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi."
Wakolosai 3:12-13
Mambo haya machache ni kati ya mengi ambayo yanaweza kufanya mahusiano ama ndoa yako idumu na iwe TAMU na yenye FURAHA siku zote za maisha yenu.
MUHIMU:
⏱️Mahusiano ni hiyari na ndoa ni hiyari. Hivyo, usilazimishe mahusiano wala ndoa na mtu ambaye hayupo tayari kwa wakati huo. Mwombe Meenyezi MUNGU kisha acha muda uamue kuwa ni nani na ni lini utaishi katika NDOA yenye FURAHA.
#No_learnig_No_earning
So we have to Learn.
Prepared By
Mr George Francis
Contact: 0713736006
EMAIL: mr.georgefrancis21@gmail.com